Loading...
ADVERTISE WITH US ON THIS BLOG.CALL +255 714 789 592/ +255 682 997 767/ +255 752 944 022

#Timu Ya Soka Ya Halmashauri Ya Mji Wa #Masasi Yapoteza Mechi Yake Ya Kirafiki Dhidi Ya #JWTZ Kambi Ya Masasi.


Na Clarence Chilumba,Masasi TC.
TIMU ya soka ya Halmashauri ya Mji wa Masasi (MASASI TC FC) kwa mara nyingine tena imeshindwa kuibuka kidedea katika mechi zake za kirafiki ambazo timu hiyo imekuwa ikicheza kwa siku za hivi karibuni lengo likiwa ni kudumisha amani,kuburudisha pamoja na kudumisha undugu baina yao na taasisi nyingine zilizopo mjini humo.

Katika mechi iliyochezwa leo katika uwanja wa Boma mjini Masasi,Timu hiyo ilijikuta ikiambulia kichapo kutoka kwa Vijana wa JWTZ Kambi ya Masasi ambao walifanikiwa kuifunga Masasi FC magoli matatu (3) kwa sifuri (0).

Mechi hiyo iliyoshuhudiwa na mashabiki Lukuki ilianza kwa kasi huku kila timu ikijaribu kupata bao la kuongoza lakini hali haikuwa hivyo mara baada ya timu zote kumaliza kipindi cha kwanza zikiwa hazijafungana.

Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko kadhaa lakini mabadiliko hayo yalionekana kuwabeba zaidi timu ya JWTZ ambayo ilifanikiwa kupata bao kunako dakika ya 50 ya kipindi hiko cha pili na kuwafanya wapinzani wao Masasi TC FC kupigana katika kutafuta bao la kusawazisha.

Licha ya wachezaji wa Masasi TC kucheza kwa “JIHADI” kutafuta bao la kusawazisha na bao la kuongoza hali ilikuwa tofauti baada ya JWTZ kujipatia mabao mawili ya harakaharaka na kufanikiwa kuongoza kwa jumla ya magoli matatu bila majibu kutoka kwa wapinzani wao.

Mechi hiyo iliyokuwa kali na ya kusisimua iliisha kwa JWTZ kambi ya Masasi kupata ushindi wa mabao matatu kwa sifuri na kuifanya Timu ya Masasi TC kupoteza mechi ya Pili mfululizo kwani katika mechi iliyopita walifungwa kwa Tabu na Masasi Veterans.

  KIKOSI cha Timu ya Halmashauri ya Mji wa Masasi

 KIKOSI cha Timu ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Kambi ya Masasi.
 BAADHI ya wapenzi na mashabiki wa Timu ya Halmashauri ya Mji wa Masasi wakifuatilia Mechi.





 WACHEZAJI wa Timu ya Masasi TC wakiwa katika  mapumziko


MASASI TC FC YAFUNGWA KWA TAABU NA MASASI VETERANS,MASHABIKI WASHUHUDIA KANDANDA SAFI

 Baadhi ya wachezaji wa Halmashauri ya mji wa Masasi wakiwa kwenye viwanja vya Boma mjini Masasi wakati wa mechi kati yao na Masasi Veterans.

Timu ya Halmashauri ya mji wa Masasi mkoani Mtwara hii leo imefungwa kwa tabu na timu ya Masasi Veterans ya mjini Humo katika mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye uwanja wa Boma mjini Masasi.

Mechi hiyo iliyoanza kwa mashambulizi kwa timu zote ilimalizika kwa Masasi Veterans kuibuka kwa ushindi wa mabao matatu bila majibu.


MECHI YA KIRAFIKI KATI YA HALMASHAURI YA MJI MASASI NA NACHINGWEA KUPIGWA 18/03/2016 UWANJA WA BOMA MJINI MASASI.

MKURUGENZI wa Halmashauri ya mji wa Masasi Fortunatus Mathew Kagoro.
TANGAZO
WANANCHI WOTE WA MJI WA MASASI PAMOJA NA WAPENZI WA MICHEZO MNAALIKWA KUHUDHURIA MCHEZO WA KIRAFIKI KATI YA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA MJI WA MASASI NA WALE WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NACHINGWEA.

MICHEZO ITAKAYOHUSIKA SIKU HIYO NI PAMOJA NA   MPIRA WA MIGUU, MIKONO PAMOJA NA MBIO NA KUVUTA KAMBA.

MECHI HIYO ITAFANYIKA SIKU YA IJUMAA TAREHE 18/03/2016 KUANZIA SAA 10:00 JIONI UWANJA WA BOMA MJINI   MASASI.

AIDHA WACHEZAJI NA MASHABIKI WA HALMASHAURI YA MJI WA MASASI MNATAKIWA KUHUDHURIA MAZOEZI AMBAYO TAYARI YAMESHAANZA SIKU KADHAA ZILIZOPITA.

MAZOEZI HAYA YANAFANYIKA KILA SIKU KUANZIA SAA 11. 00 JIONI UWANJA WA BOMA.

KUMBUKA MICHEZO HUJENGA AFYA, KUBURUDISHA PAMOJA NA KUIMARISHA “MAHUSIANO” MIONGONI MWA WANAMICHEZO.

KIINGILIO NI MACHO NA MIGUU YAKO.

WOTE MNAKARIBISHWAAAAAAAA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Adolfina Hamis,
Ofisa Michezo Halmashauri ya mji,
MASASI.
15/03/2016.

Waziri Nape amvua madaraka Mtendaji Mkuu wa Baraza la Michezo (BMT)

WAZIRI Nape Nnauye akiongea

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye amemvua madaraka Mtendaji Mkuu wa Baraza la Michezo (BMT), Henry Lihaya kwa kushindwa kutimiza wajibu wake wa kusaidia maendeleo ya michezo nchini.

Mhe. Nnauye alisema kuwa kama baraza hilo likitimiza wajibu wake linaweza kusaidia kukua kwa michezo lakini kasi ya michezo nchini inazidi kushuka na kutokana na wadau wa michezo kukosa pa kuelezea hisia zao hali inazidi mbaya zaidi.

“Nimefika ofisini hapa hata kibao kuonyesha kama hii ni ofisi ya Baraza la Michezo hakuna na hata hali ya utendaji wa kazi inaonyesha kuwa chini kama mkifanya kazi vizuri hata michezo itakua,” alisema Mhe. Nnauye.

Hivyo kutokana na sababu hiyo, Mhe. Nnauye amemvua madaraka Mtendaji Mkuu wa Baraza la Michezo (BMT) na kumwagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Elisante Oli Gabriel kumpangia kazi nyingine mtendaji mkuu huyo wizarani.

Pia kwa kanuni ya Baraza la Michezo, kifungu cha 5 (1) inamtaka Mwenyekiti wa Baraza kumchagua Mtendaji Mkuu na katika hilo Waziri Nnauye amemtaka Mwenyekiti wa Baraza la Michezo, Dionis Malinzi kupendekeza majina ya watu ambao anataka wachukue nafasi ya utendaji mkuu kisha wizara itachagua Mtendaji Mkuu mpya.

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: THE GUNNERS USO KWA USO NA BARCELONA,CHELSEA MIKONONI MWA PSG

Arsenal ya Uingereza imepangwa na Barcelona ya Uhispania kwenye hatua ya 16 bora Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Wenzao kutoka Uingereza Chelsea wamepewa miamba wa Ufaransa Paris Saint Germain baada ya droo kufanywa mjini Nyon, Uswisi.
Droo kamili:
§  Benfica (Ureno) v Zenit St Petersburg (Urusi)
§  Dynamo Kyiv (Ukraine) v Manchester City (Uingereza)
§  Juventus (Italia) v Bayern Munich (Ujerumani)
§  PSV (Uholanzi) v Atletico Madrid (Uhispania)
§  PSG (Ufaransa) v Chelsea (Uingereza)
§  Arsenal (Uingereza) v Barcelona (Uhispania)
§  Gent(Ubelgiji) v Wolfsburg(Ujerumani)

§  Roma (Italia) v Real Madrid (Uhispania)

BREAKING NEWS: JURGEN KLOPP MENEJA MPYA LIVERPOOL ASAINI KANDARASI YA MIAKA MITATU

Kocha Jurgen Klop aliyewahi kuifundisha klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani.


Klabu ya Liverpool ya jijini London Uingereza imekamilisha kandarasi ya miaka mitatu (03) ya kocha Jurgen Klop atakayeifundisha klabu hiyo katika kipindi hicho cha miaka mitatu.

Kandarasi hiyo imekuja baada ya klabu ya Liverpool kumtimua meneja wake Brendan Rodgers kwa kile kilichofafanuliwa kuwa ni kushindwa kwa meneja huyo kufanya vizuri katika michuano ya ligi kuu ya nchini uingereza pamoja na ile ya klabu bingwa Ulaya.

BONANZA LA MICHEZO LAFANYIKA MASASI,WAKURUGENZI WAOMBWA KUIPA KIPAOMBELE SEKTA YA MICHEZO

 kikosi cha Timu ya watumishi wa idara mbalimbali katika Halmashauri ya wilaya ya Masasi ambayo ilishiriki mchezo wa mpira wa miguu katika bonanza maalumu lililofanyika kwenye viwanja vya sekondari ya Ndanda mwishoni mwa wiki.


Na Clarence Chilumba, Masasi.
MKURUGENZI mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Masasi mkoani Mtwara Beatrice Dominick amewaomba wakurugenzi wa halmashauri pamoja na taasisi zingine nchini kutekeleza kwa vitendo sera ya elimu kuhusu michezo ili kudumisha ushirikiano miongoni mwa watendaji wa serikali.

Aliyasema hayo jana wakati anafanya mahojiano maalumu na habari leo kwenye uzinduzi wa bonanza la michezo lililofanyika kwenye viwanja vya shule ya sekondari Ndanda ambapo alisema lengo la bonanza hilo ni kundeleza mahusiano ya kada mbalimbali kwenye halmashauri hiyo.

Katika bonanza hilo kuwahi kutokea kwa siku za hivi karibuni wilayani Masasi liliwashirikisha wakuu wa idara na vitengo wa halmashauri hiyo,maofisa watendaji wa kata tano  zilizo jirani na shule hiyo,wanafunzi,walimu pamoja na watumishi  wa shule ya sekondari ya Ndanda huku michezo mbalimbali ikishindaniwa.

Alisema bonanza hilo ni mwanzo mzuri kwao kwani hata wale watumishi ambao kwa namna moja ama nyingine walitofautiana wakiwa kazini walipata muda wa kushirikiana pamoja kwenye michezo mbalimbali na kwamba kwa kufanya hivyo ni dhahiri bonanza hilo limesaidia kuzika rasmi tofauti za baadhi ya watendaji wa halmashauri hiyo.

 Mgeni rasmi katika Bonanza la michezo la watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Masasi ambaye ni Ofisa wa Kikosi cha kuzuia na kupambana na Rushwa wilaya ya Masasi Bw.Nestory Gatawa(kulia) akimkabidhi kikombe mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Masasi Beatrice Dominick kwenye bonanza hilo.

KAMANDA wa kikosi cha kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU wilaya ya Masasi Nestory Gatawa akizungumza wakati anafunga bonanza la michezo lililofanyika kwenye viwanja vya shule ya sekondari ya Ndanda.

Akizungumza kamanda wa kikosi cha kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) wilaya ya Masasi Nestory Gatawa alisema wadau wa michezo wanapaswa kuiga mfano uliooneshwa na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Masasi kwa kufanya matamasha na mabonanza ya michezo yenye lengo la kuimarisha ushirikiano.

Alisema kupitia bonanza hilo watendaji wa serikali wa halmashauri hiyo wamepata fursa ya kuwa pamoja na maofisa kadhaa wa Takukuru wilayani humo huku akikiri kuwa watendaji wengi wa serikali wamekuwa na dhana kuwa Takukuru ni maofisa ambao hupaswi kuwa nao karibu.

Kwa mujibu wa Gatawa alisema Takukuru ni kama taasisi zingine za serikali na kwamba watendaji wa serikali na wananchi waondoe hofu na mashaka juu ya taasisi hiyo huku akisisitiza kuwa michezo nao husaidia harakati za kupoambana na rushwa kwa kutoa elimu kupitia klabu za wapinga rushwa zilizopo mashuleni.

 Baadhi ya washiriki wakiwa kwenye bonanza hilo la michezo na hapa ni mchezo wa kunywa soda kwa haraka.

Kwa upande wake mkuu wa shule ya sekondari ya Ndanda Morega Mongate ambaye ndiye muandaaji wa bonanza hilo alisema serikali imekuwa ikihimiza michezo mashuleni katika kutekeleza dhana nzima ya michezo mashuleni iliyopo kwenye sera ya elimu ili kuibua vipaji vya michezo nchini.

Alisema licha ya changamoto ya rasilimali fedha iliyopo kwenye shule nyingi nchini lakini wakuu wa shule wanapaswa kuwa wabunifu katika kuhakikisha wanapata fedha za kuandaa mabonanza kama hayo kwa kuwa kupitia michezo wanafunzi hupata fursa ya kujifunza masuala mbalimbali ya msingi ikiwemo kudumisha ushirikiano.


Aidha aliwaomba wakuu wa shule nchini kuwa na mpango maalumu kuhusu michezo ili wanafunzi waweze kushiriki kikamilifu katika michezo mbalimbali huku akitiolea mfano kuwa katika shule yao wamekuwa na utaratibu wa kuandaa mashindano ya mabweni, madarasa pamoja nay a kutafuta vipaji vya wanafunzi katika michezo mbalimbali.


 Ofisa elimu sekondari Halmashauri ya wilaya ya Masasi Paula Nkane (kushoto) akicheza mchezo wa "MDAKO' na Ofisa elimu Msingi wa Halmashauri ya wilaya ya Masasi Bi.Editha Fue wakati wa bonanza la michezo lililofanyika huko Ndanda mwishoni mwa wiki.



Mwalimu Jane Mbunda ambaye ni mwalimu mkuu wa shule ya msingi Njenga halmashauri ya wilaya ya Masasi alikuwa ni miongoni mwa washiriki wa bonanza hilo alisema amefarijika kushiriki kwenye bonanza hilo kwani limesaidia kujenga mahusiano mazuri sambamba na kuimarisha afya za watumishi wa halmashauri hiyo.




 Timu za mpira wa miguu zikiwa zinajiandaa kabla ya kuanza mchezo huo.


KOMBE LA RPC MKOA WA LINDI LAFIKIA TAMATI,MTANDA FC MABINGWA WAPYA YAIPA KICHAPO MSINJAHILI FC

Kamanda wa polisi mkoa wa Lindi Renatha Mzinga.
Na: Mwandishi wetu,Lindi.
Timu ya mpira wa miguu ya Mtandi imefanikiwa kutwaa kombe la RPC mkoa wa Lindi Renatha Mzinga  baada ya kuifunga timu ya msinjahili mabao 2 bila majibu  katika mchezo wa fainali uliofanyika kwenye uwanja vya Ilulu mjini lindi.

Mashindano ya kombe la RPC yalianza yakiwa  na timu 19  kutoka kata 19 za Manispaa ya Lindi na moja ikiwa  ni timu ya jeshi la polisi hata hivyo chache zilifanikiwa kuingia nusu fainali na hatimaye tatu kuingia fainali.

Akizungumza katika fainali za mashindano hayo Mgeni rasmi ambaye ni  ofisa elimu wa mkoa wa Lindi Gifti Kyando alilipongeza  jeshi la polisi kwa kuanzisha mashindano hayo ambayo yatasaidia kukuza vipaji vya wachezaji hao na hatimaye Taifa kuweza kuwa na vipaji vinavyoweza kusaidia kwenye timu ya Taifa.

Kwa upande wake kocha wa timu ya Mtandi Devis Sabayo pamoja na nahodha wa timu hiyo Fadhili Hamisi walisema mashindano hayo ni muhimu kwao kwa kuwa yamewasaidia katika kuimarisha afya zao pamoja na kujenga mahusiano mazuri miongoni mwao huku wakitoa wito kwa waandaaji kutoacha kufanya hivyo kila mara.

Katika mashindano hayo timu ya Mtandi ilifanikiwa kujinyakulia  kikombe pamoja na fedha shilingi Milioni Moja, mshindi wa pili Msinjahili ilipata shilingi laki tano wakati mshindi watatu alifanikiwa kupata fedha shilingi laki tatu.

Mashindano hayo yalifunguliwa tarehe 25-07-2015 na kumalizika 25-08-2015 siku ambayo jeshi la polisi lilianzishwa nchini, ambayo katika kipindi chote cha mashindano yalivuta hisia za wakazi wa mji wa Lindi ambao walifurika katika viwanja hivyo kushuhudia.

Mwisho 

HII NI ISHARA KUBWA TOSHA KUWA SAFARI YA DE GEA IKO MBIONI KUKAMILIKA KWENDA REAL MADRID

Pereira
Goli kipa wa Manchester united ambae amechukua namba ya David De Gea ameongeza mkataba na Manchester united. Kipa huyo ame-post picha na kuandika “work harder than ever”.
Wakati David De Gea hakucheza kwenye mechi ya jana na kipa huyu amesaini mkataba ambao haujajulikana ni wa muda gani lakini wachambuzi wa mambo wanasema hali sio nzuri kwa De Gea au akipewa namba hatafanya makosa ili kutetea namba yake.
Pereira amesema kwamba ana furaha kuongeza mkataba mpya na Manchester united na pia anataka kufanya kazi kwa bidii zaidi ya zamani.
Older Posts
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top