TANGAZO
Na Clarence Chilumba,Masasi TC.
TIMU ya soka ya Halmashauri
ya Mji wa Masasi (MASASI TC FC) kwa mara nyingine tena imeshindwa kuibuka
kidedea katika mechi zake za kirafiki ambazo timu hiyo imekuwa ikicheza kwa
siku za hivi karibuni lengo likiwa ni kudumisha amani,kuburudisha pamoja na kudumisha
undugu baina yao na taasisi nyingine zilizopo mjini humo.
Katika mechi iliyochezwa
leo katika uwanja wa Boma mjini Masasi,Timu hiyo ilijikuta ikiambulia kichapo
kutoka kwa Vijana wa JWTZ Kambi ya Masasi ambao walifanikiwa kuifunga Masasi FC
magoli matatu (3) kwa sifuri (0).
Mechi hiyo iliyoshuhudiwa
na mashabiki Lukuki ilianza kwa kasi huku kila timu ikijaribu kupata bao la
kuongoza lakini hali haikuwa hivyo mara baada ya timu zote kumaliza kipindi cha
kwanza zikiwa hazijafungana.
Kipindi cha pili timu zote
zilifanya mabadiliko kadhaa lakini mabadiliko hayo yalionekana kuwabeba zaidi
timu ya JWTZ ambayo ilifanikiwa kupata bao kunako dakika ya 50 ya kipindi hiko
cha pili na kuwafanya wapinzani wao Masasi TC FC kupigana katika kutafuta bao
la kusawazisha.
Licha ya wachezaji wa
Masasi TC kucheza kwa “JIHADI” kutafuta bao la kusawazisha na bao la kuongoza
hali ilikuwa tofauti baada ya JWTZ kujipatia mabao mawili ya harakaharaka na
kufanikiwa kuongoza kwa jumla ya magoli matatu bila majibu kutoka kwa wapinzani
wao.
Mechi hiyo iliyokuwa kali na
ya kusisimua iliisha kwa JWTZ kambi ya Masasi kupata ushindi wa mabao matatu
kwa sifuri na kuifanya Timu ya Masasi TC kupoteza mechi ya Pili mfululizo kwani
katika mechi iliyopita walifungwa kwa Tabu na Masasi Veterans.
KIKOSI cha Timu ya Halmashauri ya Mji wa Masasi
KIKOSI cha Timu ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Kambi ya Masasi.
BAADHI ya wapenzi na mashabiki wa Timu ya Halmashauri ya Mji wa Masasi wakifuatilia Mechi.
WACHEZAJI wa Timu ya Masasi TC wakiwa katika mapumziko
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD