TANGAZO
WAZIRI Nape Nnauye akiongea
Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye amemvua madaraka Mtendaji Mkuu wa
Baraza la Michezo (BMT), Henry Lihaya kwa kushindwa kutimiza wajibu wake wa
kusaidia maendeleo ya michezo nchini.
Mhe. Nnauye alisema kuwa kama baraza hilo likitimiza wajibu wake linaweza
kusaidia kukua kwa michezo lakini kasi ya michezo nchini inazidi kushuka na
kutokana na wadau wa michezo kukosa pa kuelezea hisia zao hali inazidi mbaya
zaidi.
“Nimefika ofisini hapa hata kibao kuonyesha kama hii ni ofisi ya Baraza
la Michezo hakuna na hata hali ya utendaji wa kazi inaonyesha kuwa chini kama
mkifanya kazi vizuri hata michezo itakua,” alisema Mhe. Nnauye.
Hivyo kutokana na sababu hiyo, Mhe. Nnauye amemvua madaraka Mtendaji Mkuu
wa Baraza la Michezo (BMT) na kumwagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Elisante Oli Gabriel kumpangia kazi nyingine
mtendaji mkuu huyo wizarani.
Pia kwa kanuni ya Baraza la Michezo, kifungu cha 5 (1) inamtaka
Mwenyekiti wa Baraza kumchagua Mtendaji Mkuu na katika hilo Waziri Nnauye
amemtaka Mwenyekiti wa Baraza la Michezo, Dionis Malinzi kupendekeza majina ya
watu ambao anataka wachukue nafasi ya utendaji mkuu kisha wizara itachagua
Mtendaji Mkuu mpya.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD