Loading...
Home » Posts filed under News
Halmashauri ya Mji Masasi Kukutana na Wamiliki Wa Mabanda Ya Biashara "SOKOSELA" Jumatano Agosti 24,2016.
Muonekano Mpya wa Mji wa Masasi.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
HALMASHAURI YA MJI MASASI
TANGAZO KWA WAMILIKI WA MABANDA YA SOKO LA SOKOSELA
MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI WA MASASI MKOANI MTWARA, ANAWATANGAZIA WAMILIKI WOTE WA MABANDA YA BIASHARA YALIYOPO KATIKA SOKO LA SOKOSELA MAENEO YA WAPIWAPI KUFIKA KWENYE MKUTANO WA HADHARA UTAKAOFANYIKA SIKU YA JUMATANO AGOSTI 24, 2016.
MKUTANO HUO MAALUMU UTAFANYIKA KUANZIA SAA 4:00 ASUBUHI NDANI YA SOKO
HILO,AMBAPO WAMILIKI WOTE PAMOJA NA WAFANYABIASHARA WALIOHAMISHIWA KWENYE ENEO
HILO WANAPASWA KUHUDHURIA BILA KUKOSA.
MALENGO YA MKUTANO HUO NI KUTAKA KUWATAMBUA WAMILIKI WA MABANDA HAYO
AMBAYO MENGI HAYAJAENDELEZWA KWA MUDA MREFU AMBAPO WATAPEWA MUDA WA KUYAMALIZIA
ILI YAANZE KUFANYA KAZI.
WAMILIKI WOTE WA MABANDA HAYO WANAPASWA KUFIKA BILA KUKOSA ILI KUEPUKA
USUMBUFU UNAOWEZA KUJITOKEZA KWA WALE AMBAO WATASHINDWA KUFIKA BILA YA KUWA NA
SABABU ZA MSINGI.
KAULI MBIU: “ONA AIBU KUISHI NA UCHAFU, IFANYE MASASI IWE SAFI”
Limetolewa na,
Kitengo Cha Habari na Uhusiano,
Halmashauri ya Mji,
MASASI.
Agosti 22,2016.
Filed Under:
News
Monday, 22 August 2016
ZOEZI LA KUONDOA MABANDA YA BIASHARA YASIYO RASMI MJINI MASASI KUENDELEA JUMATANO 17/08/2016
![]() |
Moja ya maeneo ya Mji wa Masasi. |
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
HALMASHAURI YA MJI MASASI
TAARIFA KWA UMMA KUPITIA VYOMBO VYA HABARI
MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI WA MASASI BI.GIMBANA EMANUEL NTAVYO ANAWATANGAZIA WAFANYABIASHARA WOTE WALIOPANGA BIASHARA ZAO PEMBEZONI MWA BARABARA KUU YA MTWARA-MASASI ZIKIWEMO SARUJI,CHUMVI,NGUO,SOFA,TOFALI NA NYINGINEZO NYINGI KUWA WANATAKIWA KUONDOA BIASHARA HIZO MARA MOJA KWANI HUO NI MOJA YA UCHAFU.
MAENEO AMBAYO MABANDA YA BIASHARA YASIYO RASMI YATAONDOLEWA NI PAMOJA NA
STENDI KUU YA MABASI, ENEO LILILO NYUMA YA OFISI YA TANESCO, ENEO LILILO NYUMA
YA BENKI YA NMB NA NBC, REST CAMP, BARABARA YA NEWALA, TUNDURU, NACHINGWEA NA
BARABARA YA MTWARA/LINDI.
AIDHA MKURUGENZI WA MJI ANAWATAKA KUONDOKA MARA MOJA WATU WOTE
WANAOFANYA BIASHARA YA KUOSHA MAGARI,BAJAJ NA PIKIPIKI SEHEMU ZISIZO RASMI HASA
PEMBEZONI MWA BARABARA KUU PAMOJA NA WANAONUNUA VYUMA CHAKAVU NA KWAMBA
WATAKAOSHINDWA KUTII AGIZO HILI HALALI WATAONDOLEWA NA MAMLAKA HUSIKA.
KIKOSI KAZI KIKIONGOZWA NA OFISI YA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI WA MASASI KIMEPANGA KUENDELEA KUFANYA OPERESHENI MAALUMU KWA MARA NYINGINE ITAKAYOANZA JUMATANO AGOSTI 17,2016 YA KUONDOA VIBANDA VIDOGO VIDOGO VYA BIASHARA,WANAOOSHA MAGARI,WANAONUNUA VYUMA CHAKAVU PEMBEZONI MWA BARABARA KUU BILA YA KUPATA KIBALI KUTOKA KWA MAMLAKA HUSIKA LENGO LIKIWA NI KUUFANYA MJI WA MASASI KUWA SAFI.
OPERESHENI HII NI MAALUMU AMBAYO INALENGA KUWAONDOA WAFANYABIASHARA WOTE WANAOENDESHA BIASHARA ZAO NDANI YA MJI WA MASASI PASIPO KUFUATA UTARATIBU MAALUMU UNAOTOLEWA NA WATAALAMU WA MIPANGO MIJI WA HALMASHAURI YA MJI WA MASASI.
AIDHA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI WA MASASI ANAWAKUMBUSHA WANANCHI WOTE WA MJI WA MASASI KUWA ZOEZI LA USAFI WA MAZINGIRA LINAENDELEA NA KILELE KITAKUWA JULAI 27 AMBAPO KIMKOA KITAFANYIKA WILAYA YA MASASI KUANZIA SAA 12:00 ASUBUHI HADI SAA 4:00 ASUBUHI.
KAULI MBIU: “ONA AIBU KUISHI NA UCHAFU, IFANYE MASASI IWE SAFI”
Clarence Chilumba,
Afisa
Habari na Uhusiano,
Halmashauri
ya mji,
MASASI.
Agosti 14, 2016.
Agosti 14, 2016.
Filed Under:
News
Sunday, 14 August 2016
#Maofisa Mawasiliano Wa Serikali Nchini Watakiwa Kufanya Kazi Kimkakati Katika Utoaji Wa Taarifa Kwa Wananchi.
Waziri wa Zamani wa Habari wa Jamhuri ya Watu wa China Zhao Qizheng na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Hassan Abbas wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini, wakati wa kikao kazi cha kubadilishana uzoefu wa masuala ya Mawasiliano Serikalini, leo Jijini Dar es Salaam
Baadhi ya Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini wakimsikiliza Waziri wa Zamani wa Habari wa Jamhuri ya Watu wa China, Zhao Qizheng, wakati wa kikao kazi cha kubadilishana uzoefu wa masuala ya Mawasiliano Serikalini, Leo Jijini Dar es Salaam
Maafisa Mawasiliano Serikalini wametakiwa
kufanya kazi zao kimkakati ili kuongeza ufanisi katika utendaji wao hasa kwenye
kipindi hiki cha Awamu ya Tano.
Akizungumza
leo Jijini Dar es salaam na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini wa
Wizara na Taasisi za Serikali Waziri wa zamani wa Habari wa Jamhuri ya watu wa
China, Mhe. Zhao Qizheng amesema ni muhimu kwa Serikali kuhakikisha kuwa
mawasiliano yote yanalenga kuwainua wananchi wake.
“Msemaji
wa Serikali inabidi uwe makini katika kazi zako kwa kutoa taarifa sahihi na kwa
wakati”, alisema Qizheng.
Akifafanua Mhe. Qizheng amesema kuwa ili
Tanzania Iweze kufikia maendeleo ya kweli ni muhimu kujenga mfumo dhabiti wa
Mawasiliano ya Serikali kwa Umma.
Katika kutekeleza majukumu yao Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini kama wasemaji ni lazima wawe na uelewa mpana kuhusu masuala yanayohusu sekta wanazosimamia ili kutoa taarifa sahihi na kwa wakati kwa wananchi.
Pia aliwataka Wasemaji
wa Serikikali kujiandaa kabla ya kujibu hoja mbalimbali za kitaifa na Kimataifa
zinazohusu Serikali na wananchi ili kutoa taarifa sahihi kwa Vyombo vya habari.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Hassan Abbas amesema ni dhamira ya
Serikali kuwasiliana kimkakati ili kuchochea maendeleo.
“Lengo letu ni
Kuhakikisha kuwa tunafanya mabadiliko makubwa katika mfumo wa mawasiliano ya
Serikali na wananchi ili kuwapa fursa ya kutoa mrejesho”alisema Abbas.
Katika kuhakikisha azma
hiyo inatumia Abbas amebainisha kuwa kwa sasa Serikali inajipanga kufanya
maboresho ya mifumo ya Mawasiliano ya Serikali.
Aidha Mawasiliano ya
Serikali katika kipindi hiki cha Serikali ya awamu ya Tano yanalenga
kubadilisha maisha ya wananchi kutoka hali duni kwenda kwenye hali bora.
Mkutano kati ya Waziri
wa Zamani wa Habari wa China na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini wa
Wizara na Taasisis za Serikali umelenga kujenga uwezo wa Wasemaji wa Serikali
ili waweze kuwasiliana na Wananchi kimkakati.
Filed Under:
News
Wednesday, 10 August 2016
#MATUKIO MBALIMBALI YALIYOJIRI WAKATI WA MAONESHO YA NANE NANE VIWANJA VYA NGONGO-LINDI.
MJASILIAMALI anayefuga kuku akitoa maelezo kwa makamu wa Rais mheshimiwa Samia Suluhu Hassan wakati wa maonesho ya Nane Nane Ngongo manispaa ya Lindi.
KAMANDA wa polisi mkoa wa Lindi Renatha Mzinga akiangalia bidhaa kwenye banda la maonesho la Halmashauri ya mji ws Masasi wakati wa maonesho ya Nane Nane.
WANANCHI Waliojitokeza kwenye maadhimisho ya siku ya wakulima kwenye viwanja vya Ngongo Manispaa ya Lindi.
MKUU wa mkoa wa Lindi Mheshimiwa Godfrey Zambi akipewa maelezo kutoka kwa Afisa Kilimo wa Halmashauri ya mji wa Masasi Philipo Temba wakati wa maonesho ya Nane Nane 2016.
Filed Under:
News
Tuesday, 9 August 2016
#WAZIRI NAPE MOSES NNAUYE AIPONGEZA KAMPUNI YA MAGAZETI YA SERIKALI KUSHIRIKI NANE NANE
WAZIRI Wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mheshimiwa Nape Moses Nnauye akipata maelezo kutoka kwa mfanyakazi wa kampuni ya magazeti ya serikali.
WAZIRI wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akiwa kwenye Banda la Kampuni ya magazeti ya serikali kwenye maonesho ya Nane Nane yaliyofanyika kwenye viwanja vya Ngongo Manispaa ya Mji wa Lindi.
Baadhi ya Watumishi wa kampuni ya magazeti ya serikali wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mheshimiwa waziri Nape Moses Nnauye.
WAZIRI Nape Moses Nnauye akisaini Kitabu cha wageni kwenye banda la maonesho ya Nane Nane 2016.
MKUU wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi (Kushoto), akiagana na waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo mheshimiwa Nape Moses Nnauye.
Filed Under:
News
SERIKALI YAPIGA MARUFUKU UCHOMAJI MOTO MISITU KWA WANANCHI WA MIKOA YA LINDI NA MTWARA.
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwahutubia wakulima na wananchi kwa ujumla wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya wakulima Kitaifa yaliyofanyika Ngongo Manispaa ya mji wa Lindi.
Na Clarence Chilumba,Lindi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hasani amepiga marufuku
uchomaji moto wa misitu katika mikoa ya Lindi na Mtwara lengo likiwa ni
utunzaji wa mazingira.
Pia amewaagiza wakurugenzi
wa Halmashauri katika mikoa hiyo kuhakikisha wanawasimamia wananchi wao katika
kuachana na vitendo vya uchomaji wa misitu.
Marufuku
hiyo ameitoa leo kwenye kilele cha siku ya wakulima (NANE NANE) kwenye viwanja
vya Ngongo Manispaa ya Mji wa Lindi.
Mbunge wa jimbo la Mtwara Vijijini Mheshimiwa Hawa Ghasia (Kulia) akicheza ngoma na kikundi cha Ngoma wakati wa maadhimisho ya siku ya wakulima.
MAKAMU wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti es Halmashauri ya Mji wa Masasi Mheshimiwa Sospeter Nachunga kwenye maonesho ya Nane Nane kitaifa 2016.
WAZIRI wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Charles Tizeba akizungumza na wananchi wa Mikoa ya Lindi na Mtwara Kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wakulima kitaifa yaliyofanyika viwanja vya Ngongo Manispaa ya Lindi.
WANANNCHI wakisikiliza kwa makini Hotuba Mbalimbali za Viongozi katika maadhimisho ya siku ya wakulima.
WAZIRI wa Fedha Dk.Philip Mpango akiongea na wakazi wa mikoa ya Lindi na Mtwara.
Filed Under:
News
Monday, 8 August 2016
#Kama Hauko Ngongo Lindi,Usiangaike Nimekuwekea Matukio ktk picha ya Maonesho ya Nane Nane.
![]() |
WAZIRI george Simbachawene akiwa na mkuu wa mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Halima Dendego pamoja na Mkuu wa wilaya ya Newala. |
![]() |
Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI George Simbachawene akionesha mkoba aliopewa kwenye banda la mfuko wa Afya ya Jamii (NHIF) Kwenye banda lao la maonesho ya Nane Nane. |
![]() |
Waziri wa TAMISEMI akisaini kitabu cha wageni kwenye banda la maonesho la Halmashauri ya wilaya ya Lindi. |
![]() |
MKULIMA wa Mihogo kutoka kijiji cha Mtama mkoani Lindi Rashid Chilumba akionesha bidhaa zake kwenye maonesho ya Nane Nane. |
![]() |
WATAALAMU wa TANESCO wakitoa Elimu kwa Vitendo namna ya Kumuokoa mtu alioyepatwa na tatizo la Umeme. |
![]() |
Banda la kuku la maonesho ya Nane Nane likiwa kwenye viwanja vya Ngongo manispaa ya Lindi. |
Afisa Habari na Uhusiano wa Halmashauri ya Mji wa Masasi Bwana Clarence Chilumba,(Kulia) akitoa maelezo mafupi ya ukaribisho kwenye Banda la Maonesho la Halmashauri ya Mji wa Masasi kwa mkuu wa mkoa wa Lindi Mheshimiwa Godfrey Zambi alipotembelea banda hilo la maonesho.
MKUU wa mkoa wa Lindi akiwa ndani ya Banda la Halmashauri ya Mji wa Masasi akikagua bidhaa mbalimbali zilizopo kwenye banda hilo.
Mheshimiwa Godfrey Zambi akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wajasiliamali kwenye banda la maonesho ya Nane Nane Halmashauri ya mji wa Masasi.
MKUU wa mkoa wa Lindi Mheshimiwa Godfrey Zambi akikagua bidhaa kwenye banda la maonesho ya Nane Nane Halmashauri ya mji wa Masasi.
Filed Under:
News
Friday, 5 August 2016