TANGAZO
Kamanda wa polisi mkoa wa Lindi Renatha Mzinga. |
Na: Mwandishi wetu,Lindi.
Timu ya mpira wa miguu ya Mtandi imefanikiwa kutwaa
kombe la RPC mkoa wa Lindi Renatha Mzinga baada ya kuifunga timu ya msinjahili mabao 2
bila majibu katika mchezo wa fainali uliofanyika
kwenye uwanja vya Ilulu mjini lindi.
Mashindano ya kombe la RPC yalianza yakiwa na timu 19
kutoka kata 19 za Manispaa ya Lindi na moja ikiwa ni timu ya jeshi la polisi hata hivyo chache
zilifanikiwa kuingia nusu fainali na hatimaye tatu kuingia fainali.
Akizungumza katika fainali za mashindano hayo Mgeni
rasmi ambaye ni ofisa elimu wa mkoa wa
Lindi Gifti Kyando alilipongeza jeshi la
polisi kwa kuanzisha mashindano hayo ambayo yatasaidia kukuza vipaji vya
wachezaji hao na hatimaye Taifa kuweza kuwa na vipaji vinavyoweza kusaidia
kwenye timu ya Taifa.
Kwa upande wake kocha wa timu ya Mtandi Devis Sabayo
pamoja na nahodha wa timu hiyo Fadhili Hamisi walisema mashindano hayo ni
muhimu kwao kwa kuwa yamewasaidia katika kuimarisha afya zao pamoja na kujenga
mahusiano mazuri miongoni mwao huku wakitoa wito kwa waandaaji kutoacha kufanya
hivyo kila mara.
Katika mashindano hayo timu ya Mtandi ilifanikiwa
kujinyakulia kikombe pamoja na fedha
shilingi Milioni Moja, mshindi wa pili Msinjahili ilipata shilingi laki tano
wakati mshindi watatu alifanikiwa kupata fedha shilingi laki tatu.
Mashindano hayo yalifunguliwa tarehe 25-07-2015 na
kumalizika 25-08-2015 siku ambayo jeshi la polisi lilianzishwa nchini, ambayo
katika kipindi chote cha mashindano yalivuta hisia za wakazi wa mji wa Lindi
ambao walifurika katika viwanja hivyo kushuhudia.
Mwisho
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD