Loading...
ADVERTISE WITH US ON THIS BLOG.CALL +255 714 789 592/ +255 682 997 767/ +255 752 944 022

NIMEKUWEKEA HAPA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ZOEZI LA MADAWATI HALMASHAURI YA MJI WA MASASI.

Mojawapo ya Kituo kilchotumika katika Utengenezaji wa Madawati Halmashauri ya Mji wa Masasi.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

HALMASHAURI YA MJI MASASI
 ZOEZI LA UTENGENEZAJI WA MADAWATI 2016

TAARIFA KWA UMMA KUPITIA VYOMBO VYA HABARI

Halmashauri ya mji Masasi ni moja ya halmashauri 9 zilizopo katika mkoa wa Mtwara. Masasi Mji ina jumla ya shule za msingi 33 za serikali na 2 za binafsi. Pia kuna shule za sekondari 9 za serikali na 1 ya binafsi. Kati ya shule hizo kuna sekondari 1 ya bweni ya wasichana .Shule za serikali za msingi zina jumla ya wanafunzi 18305 ambapo wavulana 9065 na wasichana 9240. Ikama hii inapelekea kuwa na mahitaji ya madawati 6112 ambayo ni ya  wanafunzi watatu kila moja. Kwa upande wa sekondari kuna wanafunzi 3664 ambapo wavulana ni 1501 na wasichana 2163 wanaofanya mahitaji ya viti 3664 na meza 3664.

 1.    UTEKELEZAJI WA AGIZO LA RAIS

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John P. Magufuli aliagiza wakuu wa mikoa wote kuhakikisha kuwa hadi kufikia juni 30, 2016 wanafunzi wote wawe wanakaa katika madawati.

· Mikakati ya Utekelezaji

Baada ya agizo hilo halmashauri ya Mji wa Masasi tulijiweka mikakati ya kuhakikisha tunaendana na muda uliopangwa kwa zoezi hili. Ifuatayo ni mikakati tuliyojiwekea;
-          Kubainisha miti iliyo ndani ya Halmashauri na kutafuta chain saw kwa ajili ya kupasua mbao na boliti zitakazosaidia katika kukarabati na kutengenezea madawati, meza na viti.
-          Kufanya vikao na watendaji wa kata ili kuwaagiza kila kata kufanya vikao na kutafuta mbinu za kutatua tatizo ndani ya kata zao kwa usimamizi wa walezi wa kata.
-          Kuwaandikia wafadhili na wadau mbalimbali ndani na nje ya Halmashauri kuomba michango yao.
-           Kuomba kibali TFS cha kupasua mbao katika msitu wa Maparawe uliopo katika hifadhi ya Taifa.
· Hatua za Utekelezaji

Zoezi la kuondoa tatizo la upungufu wa madawati, viti na meza lilianza  mwanzoni mwa April kwa kufuata hatua zifuatazo;
-          Ofisi ya mkurugenzi kupitia ofisi yake ya Utumishi na idara za Elimu msingi na Sekondari ilikaa na watendaji wa kata pamoja na waratibu elimu kata kuwaeleza ukubwa wa tatizo na kuwataka kutafuta ufumbuzi.

-          Kuandika maandiko kwa wadau mbalimbali ndani na nje ya wilaya. Zoezi hili lilifanyika na barua na maandiko yalisambazwa kwa wafanyabiashara na makampuni yaliyo ndani na nje ya halmashauri.

-          Kuomba msitu wa kupasua mbao TFS ila gharama za kulipia miti kwa mita zilikuwa kubwa sana kiasi ofisi ya mkurugenzi kushindwa kuzihimili.

-      Kukodi Chain Saw kwa upasuaji wa mbao na kupeleka shuleni ili kukarabati madawati,viti na meza mbovu shuleni. Gharama za upasuaji wa mbao na boliti zililipwa na Halmashauri. Jumla ya mbao 4074 na boliti 1310 zilipasuliwa katika zoezi hili. Mbao na boliti hizi zilitumika kukarabati meza, viti na madawati mashuleni. Pia zilitumika katika utengenezaji wa madawati ya mbao tupu na yale ya mbao na chuma. Baadhi zilitumika kutengenezea viti meza vya sekondari.
Aidha gharama za ukarabati wa madawati, viti na meza zilikuwa za shule kupitia fedha za ukarabati katika ruzuku zao shuleni. Kwa kiasi kikubwa zoezi hili lilifanikiwa kuokoa madawati 459 ya shule za msingi na takwimu zikabadilika na kuwa na upungufu wa madawati 1543 badala ya 2002 wa awali. Kwa upande wa sekondari mbao na boliti hizi zilisaidia katika ukarabati wa viti na meza 178 vilivyokuwa havitumiki.
Halmashauri iliamua kutengeneza madawati kwa kutumia vikundi mbalimbali vya ujasilia mali na viwanda vidogo. Madawati yalitengenezwa kwa awamu tatu(3). Kwanza tulitengeneza madawati 300 ya mbao tupu katika karakana ya Christopher Kirangi iliyopo Nyasa. Awamu hii iliendana na utengenezaji wa viti meza 300 katika karakana ya Hamza Nduru iliyopo Masasi mbovu. Awamu ya pili tulitengeneza madawati 300 ya mbao na mabomba mraba na viti meza 300 katika vikundi vya wajasiliamali mbalimbali. Awamu ya tatu tulitengeneza madawati 883 kwa kupitia kamati za shule zilizo na upungufu. Shule zilizokuwa na upungufu baada ya mgawo wa madawati 600 ni Mkomaindo, Mkuti, Nyasa, Maendeleo, Sabasaba na Kambarage.

·  Michango ya Wadau

Halmashauri pia iliwaandikia wadau barua za kuomba msaada wa kutengenezewa madawati. Wadau walioandikiwa ni Benki zote zilizopo wilayani Masasi, vyama vya msingi vyote, wakandarasi wote wanaofanya kazi na halmashauri, Ikoiko LTD, wafanyabiashara wakubwa wenye maduka, nyumba za kulala wageni na wa mazao hapa mjini na makundi ya vijana. Katika hili waliotusaidia ni hawa wafuatao;


NA
MHISANI ALIYECHANGIA
VIFAA
MCHANGO  Tsh.
1
VIJANA SACOS YA MASASI

95,000/=
2
WANYUMBANI CONSTRUCTION

620,000/=
3
MAKAPO CONSTRUCTION

600,000/=
4
MBARAKA BAWAZIR

100,000/=
5
DON DON LODGE

100,000/=
6
BRAVO INN

10,000/=
7
IKO IKO LTD

50,000/=
8
HAMZA NDURU

50,000/=
9
TUMIAMINIANE  AMCOS

200,000/=
10
MKARAMANI  AMCOS

53,000/=
11
MZAZI MACHOMBE
DAWATI        10

12
MUMBAKA  AMCOS
MBAO            10

BOLITI           10


13

MISITU KANDA (TFS)
DAWATI        50

MBAO          331

BOLITI         100


JUMLA
MBAO          341
BOLITI         110
DAWATI         60

1,878.000/=


2.   HALI HALISI BAADA YA UTEKELEZAJI

·         Hali ya madawati kwa sasa

Zoezi lilikamilika juni 27 baada ya Halmashauri kutengeneza madawati 1543 ya shule za msingi na viti meza 700 vya sekondari na kupokea dawati 60 toka kwa wadau na  kufuta upungufu uliopo. Jedwali lifuatalo laelezea hali halisi hadi sasa;


MAHITAJI
YALIYOPO
YALIYO KARABATIWA
YALIYO TENGENEZWA
JUMLA
MSINGI
6112
4110
459
1543
6112
SEKONDARI
3664
2886
78
700
3664

Kwa takwimu hizi Halmashauri ya Mji hatuna upungufu wowote wa madawati katika shule zetu za msingi na sekondari.

·         Gharama zilizotumika katika zoezi

Gharama za zoezi hili la kutekeleza agizo la rais zimegawanyika katika awamu mbalimbali. Jedwali lifuatalo linaeleza;

NO
MAELEZO
KIASI
1
Shughuli za upasuaji wa mbao na uchukuzi wake
14,538,200.00
2
Madawati 300 ya mbao tupu katika karakana ya Kirangi
7,500,000.00
3
Viti meza 300 vya chuma na mbao kwa ajili ya Sekondari
10,500,000.00
4
Madawati 300 ya mbao na bomba za mraba( Square pipe) + VAT
14,181,048.84
5
Viti meza 300 vya sekondari vya Square pipe na mbao + VAT
12,105,773.40
6
Madawati 883 ambapo imelipwa fedha ya ufundi tu
23,244,530.00
7
Viti meza 100 vya sekondari vya Square pipe na mbao
3,500.000.00
JUMLA
85,569,552.24


3.   HITIMISHO

Shughuli ya kutekeleza agizo la Mh. Rais ilikuwa na changamoto mbalimbali hadi kukamilika kwake. Kwanza twamshukuru mkuu wa wilaya kwa kujitoa kusimamia kwa karibu zoezi hili na pia tunawashukuru waheshimiwa madiwani wote walioongoza vikao katani kwa lengo la kutatua tatizo. Pia Idara ya Elimu kwa ujumla tunaipongeza ofisi ya Mkurugenzi na kamati mzima ya Madawati kwa ushirikiano mkubwa uliotufanya tuweze kumaliza zoezi hili zito. Mwisho tunawashukuru wadau wote waliochangia na wasiochangia ila walikuwa na nia ya kuchangia kwani mwisho wa hili ndio mwanzo wa zoezi lingine.

Imetolewa na,
Kitengo Cha Habari na Uhuisano,
Halmashauri ya Mji,
MASASI.
Agosti 13,2016.

#Ewe Mfanyabiashara Wa Mji Wa Masasi Kuwa "MJANJA WA KWANZA" Kulipa Kodi,Kwa Maendeleo Ya Halmashauri Yako.



OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
HALMASHAURI YA MJI WA MASASI.

TAARIFA KWA UMMA KUPITIA VYOMBO VYA HABARI.

MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI WA MASASI ANAWAKUMBUSHA WAFANYABIASHARA WOTE KUWA NA LESENI HAI ZA BIASHARA.

LESENI ZA BIASHARA KWA MWAKA MPYA WA SERIKALI 2016/2017 ZIMEANZA KUTOLEWA TANGU TAREHE 1/07/2016 NA KWAMBA WALE WOTE WATAKAOSHINDWA KULIPA NDANI YA SIKU 21 WATATOZWA FAINI.

KUMBUKA KUENDESHA BIASHARA BILA KUWA NA LESENI HAI NI KINYUME NA SHERIA YA LESENI ZA BIASHARA NA.25 YA MWAKA 1972 NA.3 (1, 2 & 3).

MFANYABIASHARA YEYOTE ATAKAYEBAINIKA KUFANYA BIASHARA KINYUME NA SHERIA HII ATACHUKULIWA HATUA KALI ZA KISHERIA KAMA ILIVYOAINISHWA KATIKA KIFUNGU NA.10 (1) & (2).

AIDHA,MKURUGENZI WA MJI WA MASASI ANAWAKUMBUSHA WAMILIKI WA NYUMBA ZA KULALA WAGENI (GUEST HOUSE) KUWASILISHA KODI ZAO KATIKA WIKI YA KWANZA YA KILA MWEZI.

MWISHO,WAFANYABIASHARA WOTE WANASISITIZWA KUFUATA MASHARTI YA LESENI,IKIWA NI PAMOJA NA KUWEKA LESENI ZAO SEHEMU ZA WAZI KATIKA MAENEO YAO YA BIASHARA KWANI KUTOFANYA HIVYO NI KWENDA KINYUME NA MATAKWA YA SHERIA YA LESENI KIFUNGU NA. 14 (1).

“EWE MFANYABIASHARA WA MJI WA MASASI KUMBUKA KULIPA KODI NI WAJIBU WAKO KWA MUSTAKBALI WA MJI WAKO.

Clarence Chilumba,
Ofisa Habari Halmashauri ya Mji wa Masasi
Agosti 11, 2016.



MILIONI 50 ZA KILA KIJIJI ZILIZOAHIDIWA NA DK.MAGUFULI ZAIVA,LINDI NA MTWARA KUPEWA KIPAOMBELE

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Magufuli (picha ya Maktaba)

Hatimaye serikali imetengua kitendawili cha lini ahadi ya Rais John Magufuli ya kutoa Sh. milioni 50 za maendeleo kwa kila kijiji nchini itatekelezwa, kama alivyoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana. 

Aidha, katika mpango wa utekelezaji wa ahadi hiyo, serikali imetenga Sh. bilioni 811 na imeshaanza kushirikisha wadau mbalimbali ili kupata maoni ya kuendesha mchakato huo kwa ufanisi na tija. 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam baada ya kikao cha wadau waliokuwa wakijadili rasimu ya mpango huo mwishoni mwa wiki, Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng'i Issa, alisema serikali itaanza kutoa fedha hizo kuanzia mwaka ujao wa fedha.

"Kwa kuanzia, fedha  hizo zitatolewa kwa awamu tatu katika kipindi cha miaka mitano,” alisema na kuongeza:  
"Fedha hizo zitatolewa benki kabla ya kutolewa kwa vikundi mbalimbali kama Vicoba na Saccos kulingana na taratibu zitakazowekwa."

Kwa mujibu wa mpango huo, mchakato utaanza na mikoa 10 nchini iliyo nyuma katika kutumia huduma za kifedha. Mikoa hiyo, kwa mujibu wa taarifa ya utafiti ya Finscope ya mwaka 2013 ni  Singida, Lindi, Mtwara, Mbeya, Shinyanga, Geita, Kagera, Dodoma, Rukwa na Ruvuma. 

Akifungua mkutano huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama, alisema mkutano huo ulilenga kupata maoni ya wataalamu namna bora ya kutekeleza mpango huo.

Akizungumza kwa niaba ya waziri, Kaimu Mkurugenzi, Maendeleo ya Sekta Binafsi, Uwekezaji na Uwezeshaji, Ofisi ya Waziri Mkuu, Victor Mwainyekule, alisema mawazo yaliyopatikana yatazingatiwa ili kuboresha kazi hiyo, yenye lengo la kupambana na umasikini.

Kwa upande wake, Mkuu wa Uendeshaji wa Benki ya Wanawake (TWB), Zablon Yebete, alisema mpango huo ni uwekezaji mkubwa kwa Watanzania unaopaswa kuungwa mkono na vyombo vya fedha na wadau wengine nchini.

Kwa mujibu wa mpango huo, walengwa watapatiwa mafunzo ya ujasiriamali kabla ya kupatiwa fedha.

Mkutano huo ulihudhuriwa na wawakilishi wa halmashauri za wilaya, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf), benki, mifuko ya hifadhi ya jamii na vikundi mbalimbali.

Older Posts
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top