TANGAZO
Picha ya Ng'ombe
TAARIFA YA MLIPUKO WA HOMA YA MAPAFU YA NG’OMBE
Ndugu wananchi wa mji wa
Masasi na vitongoji vyake taarifa iwafikie kwamba katikakati ya mwezi Februari
2016, kumetokea mlipuko wa Homa ya mapafu ya Ng’ombe (Contagious Bovine Pleuropneumonia)
katika kijiji cha Mkarango Halmashauri ya mji wa Masasi.
Aidha hadi Machi 01, 2016
jumla ya Ng’ombe 18 waliripotiwa kufa kutokana na ugonjwa huo katika kijiji
hiko cha Mkarango.
Ugonjwa huu ni hatari sana
na kwamba unaambukizwa kwa kasi kubwa ambapo wanyama wote jamii ya Ng’ombe (Bovine)
wakiwemo Ng’ombe,Nyati,na Nyati Maji huathiriwa na ugonjwa huu.
Ugonjwa huu wa mapafu ya Ng’ombe
unaambukizwa kwa njia ya mafua kutoka kwa wanyama wanaougua lakini pia
huambukizwa kwa njia ya mate kwa kuchangia chakula na maji yaliyochafuliwa na
vijidudu vya ugonjwa huo.
Hivyo basi kutokana na
kushambuliwa na kuathirika kwa njia ya hewa wanyama wengi walioathirika na
ugonjwa huo hufa.
DALILI ZA UGONJWA
·
Mnyama hupumua kwa shida na kukohoa.
·
Mnyama hutokwa na mafua
· Mnyama hupoteza hamu ya kula na kuonekana
kujitenga kutoka kundi kubwa.
· Mnyama aliyekufa akipasuliwa sehemu ya kifua
huonekana ikiwa imejaa maji ya rangi ya njano.
· Mapafu huonekana yakiwa yamevimba na
kubadilika rangi kama ya maini pia yanaonekana yakiwa yameganda kwenye mbavu na
kufunikwa na ute mzito wa njano.
CHANJO NA TIBA
Ugonjwa huu hauna tiba
yeyote ukishatokea bali chanjo ya kuzuia ugonjwa huo inatakiwa itolewe miezi
kadhaa kabla ugonjwa haujatokea.
Kufuatia kujiridhisa kwetu
kwamba ugonjwa huo upo baada ya taarifa kutoka kwa wafugaji wa kijiji cha
Mkarango,tumepeleka taarifa mkoani pia kwenye kituo cha uchunguzi wa magonjwa
ya mifugo (VIC) Naliendele kwa hatua zaidi za utekelezaji ili kunusuru kundi la
ng’ombe takribani 500 wa kata za Temeke,Migongo na Mwenge Mtapika lililo katika
hatua ya kuambukizwa.
NB:
Nyama ya mgonjwa aliyekufa kwa ugonjwa haina madhara yoyote kwa
binadamu.
Clarence
Antony Chilumba,
Ofisa
Habari Halmashauri ya mji wa Masasi
S.L.P.
447,
MASASI.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD