TANGAZO
Mojawapo ya Kituo kilchotumika katika Utengenezaji wa Madawati Halmashauri ya Mji wa Masasi. |
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
HALMASHAURI YA MJI MASASI
ZOEZI LA UTENGENEZAJI WA MADAWATI 2016
TAARIFA KWA UMMA KUPITIA VYOMBO
VYA HABARI
Halmashauri ya mji
Masasi ni moja ya halmashauri 9 zilizopo katika
mkoa wa Mtwara. Masasi Mji ina jumla ya shule za msingi 33 za serikali na 2 za
binafsi. Pia kuna shule za sekondari 9 za
serikali na 1 ya binafsi. Kati ya shule hizo
kuna sekondari 1 ya bweni ya wasichana .Shule za
serikali za msingi zina jumla ya wanafunzi 18305 ambapo wavulana 9065 na wasichana 9240. Ikama hii inapelekea kuwa na mahitaji ya madawati 6112 ambayo ni ya
wanafunzi watatu kila moja. Kwa upande wa sekondari kuna wanafunzi 3664 ambapo wavulana ni 1501 na
wasichana 2163
wanaofanya mahitaji ya viti 3664 na meza 3664.
1. UTEKELEZAJI
WA AGIZO LA RAIS
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dr. John P. Magufuli aliagiza wakuu wa mikoa wote
kuhakikisha kuwa hadi kufikia juni 30, 2016 wanafunzi wote wawe wanakaa katika
madawati.
· Mikakati ya Utekelezaji
Baada
ya agizo hilo halmashauri ya Mji wa Masasi tulijiweka mikakati ya kuhakikisha
tunaendana na muda uliopangwa kwa zoezi hili. Ifuatayo ni mikakati
tuliyojiwekea;
-
Kubainisha miti iliyo ndani
ya Halmashauri na kutafuta chain saw kwa ajili ya kupasua mbao na boliti
zitakazosaidia katika kukarabati na kutengenezea madawati, meza na viti.
-
Kufanya vikao na watendaji
wa kata ili kuwaagiza kila kata kufanya vikao na kutafuta mbinu za kutatua
tatizo ndani ya kata zao kwa usimamizi wa walezi wa kata.
-
Kuwaandikia wafadhili na
wadau mbalimbali ndani na nje ya Halmashauri kuomba michango yao.
-
Kuomba kibali TFS cha kupasua mbao katika
msitu wa Maparawe uliopo katika hifadhi ya Taifa.
· Hatua za Utekelezaji
Zoezi la kuondoa
tatizo la upungufu wa madawati, viti na meza lilianza mwanzoni mwa April kwa kufuata hatua
zifuatazo;
-
Ofisi ya mkurugenzi kupitia
ofisi yake ya Utumishi na idara za Elimu msingi na Sekondari ilikaa na
watendaji wa kata pamoja na waratibu elimu kata kuwaeleza ukubwa wa tatizo na
kuwataka kutafuta ufumbuzi.
-
Kuandika maandiko kwa wadau
mbalimbali ndani na nje ya wilaya. Zoezi hili lilifanyika na barua na maandiko
yalisambazwa kwa wafanyabiashara na makampuni yaliyo ndani na nje ya
halmashauri.
- Kuomba msitu wa kupasua
mbao TFS ila gharama za kulipia miti kwa mita zilikuwa kubwa sana kiasi ofisi
ya mkurugenzi kushindwa kuzihimili.
- Kukodi Chain Saw kwa
upasuaji wa mbao na kupeleka shuleni ili kukarabati madawati,viti na meza mbovu
shuleni. Gharama za upasuaji wa mbao na boliti zililipwa na Halmashauri. Jumla
ya mbao 4074
na boliti 1310
zilipasuliwa katika zoezi hili. Mbao na boliti hizi zilitumika kukarabati meza,
viti na madawati mashuleni. Pia zilitumika katika utengenezaji wa madawati ya
mbao tupu na yale ya mbao na chuma. Baadhi zilitumika kutengenezea viti meza
vya sekondari.
Aidha gharama za
ukarabati wa madawati, viti na meza zilikuwa za shule kupitia fedha za
ukarabati katika ruzuku zao shuleni. Kwa kiasi kikubwa zoezi hili lilifanikiwa
kuokoa madawati 459 ya shule za
msingi na takwimu zikabadilika na kuwa na upungufu wa madawati 1543 badala ya 2002 wa awali. Kwa upande wa sekondari mbao na boliti hizi
zilisaidia katika ukarabati wa viti na meza 178 vilivyokuwa havitumiki.
Halmashauri iliamua
kutengeneza madawati kwa kutumia vikundi mbalimbali vya ujasilia mali na
viwanda vidogo. Madawati yalitengenezwa kwa awamu tatu(3). Kwanza tulitengeneza madawati 300
ya mbao tupu katika karakana ya Christopher Kirangi iliyopo Nyasa. Awamu hii
iliendana na utengenezaji wa viti meza 300
katika karakana ya Hamza Nduru iliyopo Masasi mbovu. Awamu ya pili tulitengeneza madawati 300 ya mbao na mabomba mraba na viti
meza 300 katika vikundi vya
wajasiliamali mbalimbali. Awamu ya tatu
tulitengeneza madawati 883 kwa
kupitia kamati za shule zilizo na upungufu. Shule zilizokuwa na upungufu baada
ya mgawo wa madawati 600 ni Mkomaindo, Mkuti, Nyasa, Maendeleo, Sabasaba na
Kambarage.
· Michango
ya Wadau
Halmashauri pia
iliwaandikia wadau barua za kuomba msaada wa kutengenezewa madawati. Wadau
walioandikiwa ni Benki zote zilizopo wilayani Masasi, vyama vya msingi vyote,
wakandarasi wote wanaofanya kazi na halmashauri, Ikoiko LTD, wafanyabiashara
wakubwa wenye maduka, nyumba za kulala wageni na wa mazao hapa mjini na makundi
ya vijana. Katika hili waliotusaidia ni hawa wafuatao;
NA
|
MHISANI
ALIYECHANGIA
|
VIFAA
|
MCHANGO Tsh.
|
1
|
VIJANA SACOS YA MASASI
|
|
95,000/=
|
2
|
WANYUMBANI CONSTRUCTION
|
|
620,000/=
|
3
|
MAKAPO CONSTRUCTION
|
|
600,000/=
|
4
|
MBARAKA BAWAZIR
|
|
100,000/=
|
5
|
DON DON LODGE
|
|
100,000/=
|
6
|
BRAVO INN
|
|
10,000/=
|
7
|
IKO IKO LTD
|
|
50,000/=
|
8
|
HAMZA NDURU
|
|
50,000/=
|
9
|
TUMIAMINIANE AMCOS
|
|
200,000/=
|
10
|
MKARAMANI AMCOS
|
|
53,000/=
|
11
|
MZAZI MACHOMBE
|
DAWATI 10
|
|
12
|
MUMBAKA AMCOS
|
MBAO 10
|
|
BOLITI 10
|
|
||
13
|
MISITU KANDA (TFS)
|
DAWATI 50
|
|
MBAO 331
|
|
||
BOLITI 100
|
|
||
JUMLA
|
MBAO 341
BOLITI 110
DAWATI 60
|
1,878.000/=
|
2. HALI HALISI BAADA YA
UTEKELEZAJI
·
Hali
ya madawati kwa sasa
Zoezi lilikamilika
juni 27 baada ya Halmashauri kutengeneza madawati 1543 ya shule za msingi na
viti meza 700 vya sekondari na kupokea dawati 60 toka kwa wadau na kufuta upungufu uliopo. Jedwali lifuatalo
laelezea hali halisi hadi sasa;
|
MAHITAJI
|
YALIYOPO
|
YALIYO
KARABATIWA
|
YALIYO
TENGENEZWA
|
JUMLA
|
MSINGI
|
6112
|
4110
|
459
|
1543
|
6112
|
SEKONDARI
|
3664
|
2886
|
78
|
700
|
3664
|
Kwa takwimu hizi
Halmashauri ya Mji hatuna upungufu wowote wa madawati katika shule zetu za
msingi na sekondari.
·
Gharama
zilizotumika katika zoezi
Gharama za zoezi
hili la kutekeleza agizo la rais zimegawanyika katika awamu mbalimbali. Jedwali
lifuatalo linaeleza;
NO
|
MAELEZO
|
KIASI
|
1
|
Shughuli
za upasuaji wa mbao na uchukuzi wake
|
14,538,200.00
|
2
|
Madawati
300 ya mbao tupu katika karakana ya Kirangi
|
7,500,000.00
|
3
|
Viti
meza 300 vya chuma na mbao kwa ajili ya Sekondari
|
10,500,000.00
|
4
|
Madawati
300 ya mbao na bomba za mraba( Square pipe) + VAT
|
14,181,048.84
|
5
|
Viti
meza 300 vya sekondari vya Square pipe na mbao + VAT
|
12,105,773.40
|
6
|
Madawati
883 ambapo imelipwa fedha ya ufundi tu
|
23,244,530.00
|
7
|
Viti
meza 100 vya sekondari vya Square pipe na mbao
|
3,500.000.00
|
JUMLA
|
85,569,552.24
|
3. HITIMISHO
Shughuli
ya kutekeleza agizo la Mh. Rais ilikuwa na changamoto mbalimbali hadi
kukamilika kwake. Kwanza twamshukuru mkuu wa wilaya kwa kujitoa kusimamia kwa
karibu zoezi hili na pia tunawashukuru waheshimiwa madiwani wote walioongoza
vikao katani kwa lengo la kutatua tatizo. Pia Idara ya Elimu kwa ujumla
tunaipongeza ofisi ya Mkurugenzi na kamati mzima ya Madawati kwa ushirikiano
mkubwa uliotufanya tuweze kumaliza zoezi hili zito. Mwisho tunawashukuru wadau
wote waliochangia na wasiochangia ila walikuwa na nia ya kuchangia kwani mwisho
wa hili ndio mwanzo wa zoezi lingine.
Imetolewa na,
Kitengo Cha Habari na Uhuisano,
Halmashauri ya Mji,
MASASI.
Agosti 13,2016.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD