TANGAZO
OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
HALMASHAURI YA MJI WA MASASI.
TAARIFA KWA UMMA KUPITIA VYOMBO VYA HABARI.
MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI WA MASASI
ANAWAKUMBUSHA WAFANYABIASHARA WOTE KUWA NA LESENI HAI ZA BIASHARA.
LESENI ZA BIASHARA KWA MWAKA MPYA WA SERIKALI
2016/2017 ZIMEANZA KUTOLEWA TANGU TAREHE 1/07/2016 NA KWAMBA WALE WOTE
WATAKAOSHINDWA KULIPA NDANI YA SIKU 21 WATATOZWA FAINI.
KUMBUKA KUENDESHA BIASHARA BILA KUWA NA LESENI HAI
NI KINYUME NA SHERIA YA LESENI ZA BIASHARA NA.25 YA MWAKA 1972 NA.3 (1, 2 &
3).
MFANYABIASHARA YEYOTE ATAKAYEBAINIKA KUFANYA
BIASHARA KINYUME NA SHERIA HII ATACHUKULIWA HATUA KALI ZA KISHERIA KAMA
ILIVYOAINISHWA KATIKA KIFUNGU NA.10 (1) & (2).
AIDHA,MKURUGENZI WA MJI WA MASASI ANAWAKUMBUSHA
WAMILIKI WA NYUMBA ZA KULALA WAGENI (GUEST HOUSE) KUWASILISHA KODI ZAO KATIKA
WIKI YA KWANZA YA KILA MWEZI.
MWISHO,WAFANYABIASHARA WOTE WANASISITIZWA KUFUATA
MASHARTI YA LESENI,IKIWA NI PAMOJA NA KUWEKA LESENI ZAO SEHEMU ZA WAZI KATIKA
MAENEO YAO YA BIASHARA KWANI KUTOFANYA HIVYO NI KWENDA KINYUME NA MATAKWA YA
SHERIA YA LESENI KIFUNGU NA. 14 (1).
“EWE MFANYABIASHARA WA MJI WA MASASI KUMBUKA
KULIPA KODI NI WAJIBU WAKO KWA MUSTAKBALI WA MJI WAKO.
Clarence Chilumba,
Ofisa Habari Halmashauri ya Mji wa Masasi
Agosti 11, 2016.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD