Loading...
ADVERTISE WITH US ON THIS BLOG.CALL +255 714 789 592/ +255 682 997 767/ +255 752 944 022

ZOEZI LA KUONDOA MABANDA YA BIASHARA YASIYO RASMI MJINI MASASI KUENDELEA JUMATANO 17/08/2016

TANGAZO
Moja ya maeneo ya Mji wa Masasi.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS

TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

HALMASHAURI YA MJI MASASI 

                                                                                            

TAARIFA KWA UMMA KUPITIA VYOMBO VYA HABARI

MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI WA MASASI
BI.GIMBANA EMANUEL NTAVYO ANAWATANGAZIA WAFANYABIASHARA WOTE WALIOPANGA BIASHARA ZAO PEMBEZONI MWA BARABARA KUU YA MTWARA-MASASI ZIKIWEMO SARUJI,CHUMVI,NGUO,SOFA,TOFALI NA NYINGINEZO NYINGI KUWA WANATAKIWA KUONDOA BIASHARA HIZO MARA MOJA KWANI HUO NI MOJA YA UCHAFU.

MAENEO AMBAYO MABANDA YA BIASHARA YASIYO RASMI YATAONDOLEWA NI PAMOJA NA STENDI KUU YA MABASI, ENEO LILILO NYUMA YA OFISI YA TANESCO, ENEO LILILO NYUMA YA BENKI YA NMB NA NBC, REST CAMP, BARABARA YA NEWALA, TUNDURU, NACHINGWEA NA BARABARA YA MTWARA/LINDI.

AIDHA MKURUGENZI WA MJI ANAWATAKA KUONDOKA MARA MOJA WATU WOTE WANAOFANYA BIASHARA YA KUOSHA MAGARI,BAJAJ NA PIKIPIKI SEHEMU ZISIZO RASMI HASA PEMBEZONI MWA BARABARA KUU PAMOJA NA WANAONUNUA VYUMA CHAKAVU NA KWAMBA WATAKAOSHINDWA KUTII AGIZO HILI HALALI WATAONDOLEWA NA MAMLAKA HUSIKA.

KIKOSI KAZI KIKIONGOZWA NA OFISI YA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI WA MASASI KIMEPANGA KUENDELEA KUFANYA OPERESHENI MAALUMU KWA MARA NYINGINE ITAKAYOANZA JUMATANO AGOSTI 17,2016 YA KUONDOA VIBANDA VIDOGO VIDOGO VYA BIASHARA,WANAOOSHA MAGARI,WANAONUNUA VYUMA CHAKAVU  PEMBEZONI MWA BARABARA KUU BILA YA KUPATA KIBALI KUTOKA KWA MAMLAKA HUSIKA LENGO LIKIWA NI KUUFANYA MJI WA MASASI KUWA SAFI.

OPERESHENI HII NI MAALUMU AMBAYO INALENGA KUWAONDOA WAFANYABIASHARA WOTE WANAOENDESHA BIASHARA ZAO NDANI YA MJI WA MASASI PASIPO KUFUATA UTARATIBU MAALUMU UNAOTOLEWA NA WATAALAMU WA MIPANGO MIJI WA HALMASHAURI YA MJI WA MASASI.


AIDHA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI WA MASASI ANAWAKUMBUSHA WANANCHI WOTE WA MJI WA MASASI KUWA ZOEZI LA  USAFI WA MAZINGIRA LINAENDELEA NA KILELE KITAKUWA JULAI 27 AMBAPO KIMKOA KITAFANYIKA WILAYA YA  MASASI KUANZIA SAA 12:00 ASUBUHI HADI SAA 4:00 ASUBUHI.

KAULI MBIU: “ONA AIBU KUISHI NA UCHAFU, IFANYE MASASI IWE SAFI”

Clarence Chilumba,
Afisa Habari na Uhusiano,
Halmashauri ya mji,
MASASI.
Agosti 14, 2016.

TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top