TANGAZO
Waziri wa Zamani wa Habari wa Jamhuri ya Watu wa China Zhao Qizheng na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Hassan Abbas wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini, wakati wa kikao kazi cha kubadilishana uzoefu wa masuala ya Mawasiliano Serikalini, leo Jijini Dar es Salaam
Baadhi ya Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini wakimsikiliza Waziri wa Zamani wa Habari wa Jamhuri ya Watu wa China, Zhao Qizheng, wakati wa kikao kazi cha kubadilishana uzoefu wa masuala ya Mawasiliano Serikalini, Leo Jijini Dar es Salaam
Maafisa Mawasiliano Serikalini wametakiwa
kufanya kazi zao kimkakati ili kuongeza ufanisi katika utendaji wao hasa kwenye
kipindi hiki cha Awamu ya Tano.
Akizungumza
leo Jijini Dar es salaam na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini wa
Wizara na Taasisi za Serikali Waziri wa zamani wa Habari wa Jamhuri ya watu wa
China, Mhe. Zhao Qizheng amesema ni muhimu kwa Serikali kuhakikisha kuwa
mawasiliano yote yanalenga kuwainua wananchi wake.
“Msemaji
wa Serikali inabidi uwe makini katika kazi zako kwa kutoa taarifa sahihi na kwa
wakati”, alisema Qizheng.
Akifafanua Mhe. Qizheng amesema kuwa ili
Tanzania Iweze kufikia maendeleo ya kweli ni muhimu kujenga mfumo dhabiti wa
Mawasiliano ya Serikali kwa Umma.
Katika kutekeleza majukumu yao Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini kama wasemaji ni lazima wawe na uelewa mpana kuhusu masuala yanayohusu sekta wanazosimamia ili kutoa taarifa sahihi na kwa wakati kwa wananchi.
Pia aliwataka Wasemaji
wa Serikikali kujiandaa kabla ya kujibu hoja mbalimbali za kitaifa na Kimataifa
zinazohusu Serikali na wananchi ili kutoa taarifa sahihi kwa Vyombo vya habari.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Hassan Abbas amesema ni dhamira ya
Serikali kuwasiliana kimkakati ili kuchochea maendeleo.
“Lengo letu ni
Kuhakikisha kuwa tunafanya mabadiliko makubwa katika mfumo wa mawasiliano ya
Serikali na wananchi ili kuwapa fursa ya kutoa mrejesho”alisema Abbas.
Katika kuhakikisha azma
hiyo inatumia Abbas amebainisha kuwa kwa sasa Serikali inajipanga kufanya
maboresho ya mifumo ya Mawasiliano ya Serikali.
Aidha Mawasiliano ya
Serikali katika kipindi hiki cha Serikali ya awamu ya Tano yanalenga
kubadilisha maisha ya wananchi kutoka hali duni kwenda kwenye hali bora.
Mkutano kati ya Waziri
wa Zamani wa Habari wa China na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini wa
Wizara na Taasisis za Serikali umelenga kujenga uwezo wa Wasemaji wa Serikali
ili waweze kuwasiliana na Wananchi kimkakati.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD