TANGAZO
Na Bashiru
Kauchumbe,Ruangwa.
Serikali imesema ipo mbioni kuufanyia marekebisho mfumo wa ununuzi wa zao la korosho maarufu mfumo wa stakabadhi ghalani ili wananchi waweze kunufaika na matunda yatokanayo na zao hilo muhimu kwa uchumi wa nchi.
Hayo yamesemwa leo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe Kasimu Majaliwa ambaye yuko wilayani Ruangwa katika mkoa wa Lindi kwa Ziara
ya Kikazi aliyoianza hii leo wilayani humo. .
Alisema kuwa mfumo wa Stakabadhi ghalani umekuwa ukiwanyonya wakulima wa zao la Korosho kutokana na utendaji mbovu wa watendaji wanaosimamia mfumo huo kuanzia vyama vya msingi ,Vyama vikuu vya ushirika na Bodi ya Korosho nchini mazingira yanayosababisha wakulima wa zao hilo kubaki maskini.

Alisema katika kulitafutia
ufumbuzi suala hilo amekutana na Viongozi wa Bodi ya Korosho mapema mwaka huu
ili kuondoa baadhi ya vipengele ambavyo vinaonekana kuwanyonya na kuwakandamiza
wakulima wa zao la Korosho nchini.
Alivitaja vipengele hivyo kuwa ni pamoja na ushuru wa asilimia moja unaokwenda kwa afisa Ushirika wa Mkoa,Ushuru wa kusafirisha korosho kwenda kwenye maghala ambao ni shilingi 50 kwa kila kilo moja,makato ya shilingi 50 ya chama kikuu cha ushirika,pamoja na riba ya Mkopo wa Benki baada ya chama kupata Mkopo kutoka Benki.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu amesema kuwa hakuna haja ya kumbebesha
Mkulima kulipa gharama hizo kwani kuna baadhi ya vyama vinatumia magari ya
vyama kusafirishia korosho mpaka kwenye maghala makuu lakini mzigo wa kulipa
gharama hizo anabebeshwa Mkulima huku akiwahakikishia wananchi wilayani Ruangwa
kuwa kero hizo zitakwisha.
Akizungumzia kuhusu riba ya Mikopo ya Benki kwa vyama vya msingi
alisema sio lazima gharama hizo kufanywa
na Mkulima kwani wanaohusika kufanya Mikataba ya Mikopo hiyo ni Vyama vya msingi na
sio wakulima hivyo vyama vina wajibu wa kulipa gharama hizo.
Kwa upande wa gharama za kulipia maghala makuu amevitaka vyama vya msingi vilipe vyenyewe gharama hizo au vyama vikuu viende katika maghala ya Vyama vya msingi kwenda kununua Korosho kwa wakulima.
Zao la Korosho nchini Tanzania ni miongoni mwa zao ambalo linaongeza uchumi wa nchi ,lakini tangu kuanzishwa kwa mfumo wa Stakabadhi ghalani katika Mikoa ya Lindi na Mtwara wakulima wengi wa zao hilo wamekuwa wakilalamikia mfumo huo kutokana kuwa na makato yasiyokuwa na tija kwa wakulima ,pamoja na malipo yasiyokuwa na uhakika.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi ambaye ameambatana na Waziri Mkuu katika ziara hiyo amewataka wakulima wa zao la Korosho Mkoani Lindi kufanya palizi ya Mashamba yao mapema ili kuepusha mikorosho hiyo kuungua moto nyakati za Kiangazi.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD