TANGAZO
Na Bashiru
Kauchumbe,Ruangwa.
WANANCHI wilayani
Ruangwa mkoani Lindi wametakiwa kulima kwa wingi kilimo cha zao la muhogo lengo
likiwa ni kukuza kipato chao pamoja na uchumi wa nchi mazingira yatakayosaidia pia
kuondokana na tatizo la njaa linalotokana na mabadiliko ya hali ya hewa
yanayosababisha ukame katika baadhi ya vijiji wilayani humo.
Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ruangwa Mhe Kassimu Majaliwa kwa nyakati
tofauti alipofanya Mikutano ya hadhara katika Vijiji vya Kitandi,Nkowe na
Namahema.
Alisema kwa sasa kilimo cha Muhogo kina faida kubwa kwani wapo wafanyabiashara ambao wanataka kuwekeza katika kilimo hicho na tayari amempata mfanyabiashara wa kigeni ambaye yupo tayari kununua zao la Muhogo katika Mikoa ya Lindi na Mtwara ambapo amewataka kuongeza kasi ya uzalishaji wa zao hilo ili kukidhi mahitaji ya Mwekezaji huyo ambaye amekubali kuja kujenga kiwanda cha kusindika zao la muhogo.
Kwa mujibu wa waziri mkuu amesema kuwa huu ni wakati wa wananchi wa
wilaya ya Ruangwa kubadilika na kufanya kazi ili weweze kuendana na kasi ya
awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk.John Pombe Magufuli..
Kwa miaka ya hivi Karibuni kilimo cha zao la muhogo kilianza kutoweka baada ya wakulima kutoona faida yake huku wakazi wengi wa wilaya ya Ruangwa wakitumia zao hilo kwa ajili ya kupikia pombe wakati wa sherehe mbalimbali za kimila ikiwemo jando na unyago.
Kwa miaka ya hivi Karibuni kilimo cha zao la muhogo kilianza kutoweka baada ya wakulima kutoona faida yake huku wakazi wengi wa wilaya ya Ruangwa wakitumia zao hilo kwa ajili ya kupikia pombe wakati wa sherehe mbalimbali za kimila ikiwemo jando na unyago.
Kwa upande wao baadhi ya
wananchi wilayani Ruangwa wamepongeza hamasa na ushauri uliotolewa na Waziri
Mkuu huku wakulima wengi wakiahidi kuwa kwa
sasa watachangamkia fursa ya kulima zao la Muhogo kwa kuwa limekuwa zao la biashara.
Zao la Muhogo kwa mikoa ya Lindi na Mtwara hulimwa
zaidi katika wilaya ya Newala Mkoani Mtwara ingawa kwa sasa lipo hatarini kutoweka kutokana na wakulima
wengi kuacha kulima zao hilo na kukimbilia wilaya za Ruangwa,Kilwa na Liwale
mkoani Lindi kwa ajili ya kulima zao la
Ufuta ambalo linaonekana kuwa na soko lenye tija.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD