TANGAZO
HALMASHAURI YA MJI MASASI
Serikali kupitia bunge lake
la kumi ilipitisha kanuni za Leseni za usafirishaji wa abiria kwa njia ya
pikipiki za magurudumu mawili na matatu (The Transport Licensing (motorcycles
an tricycles) regulation 2010.
Kanuni hizo zimezipa
mamlaka za serikali za mitaa kutoa leseni za usafirishaji wa abiria kwa kutumia
pikipiki za miguu miwili na mitatu kwa makubaliano maalumu na SUMATRA
(Memorandum of Understanding)
Kufuatia makubaliano hayo Halmashauri
ya Mji Masasi inaanza kutekeleza Sheria Chini ya Kifungu 5A cha Sheria ya
SUMATRA Na. 9 ya 2001 na kanuni za Leseni za usafirishaji Pikipiki magurudumu
mawili (Bodaboda) na matatu (Bajaji) kuanzia sasa.
Leseni za usafirishaji
(SUMATRA) zinapatikana katika ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji kuanzia
sasa.
MASHARTI
YA KUPATA LESENI YA USAFIRISHAJI PIKIPIKI NA BAJAJI
1.
Barua ya maombi ya leseni (aoneshe kijiwe
anachotoka/ anachopaki)
2.
Barua ya utambulisho kutoka serikali ya
Mtaa.
3.
Nakala ya kadi ya pikipiki/ bajaji
4.
Nakala ya Bima ya pikipiki/ bajaji
5.
Nakala ya leseni ya udereva
6.
Taarifa ya ukaguzi wa chombo cha
usafirishaji kutoka polisi (vehicle inspection report)
ADA YA LESENI YA USAFIRISHAJI
1. PIKIPIKI:
Fomu ya maombi ni Tshs 2,000/= na Ada ya leseni kwa mwaka ni Tshs 20,000/=
JUMLA SHILINGI 22,000/=
2. BAJAJI:
Fomu ya maombi ni Tshs 2,000/= na Ada ya leseni kwa mwaka ni Tshs 30,000/ JUMLA SHILINGI 32,000/=
Malipo yote yanafanyika
katika ofisi ya Mkurugenzi wa Mji Masasi.
VIJIWE
VINAVYOTAMBULIKA MPAKA SASA NI VIFUATAVYO;
1. Resti
camp, Mkomaindo na barabara ya Tunduru
2. Eneo
la Stendi na barabara ya Nachingwea
3. Eneo
la Mkuti sokoni, kaumu, eneo la machinjioni
4. Jida
na mtandi
5. TK,
eneo la Nyasa Magengeni na Barabara ya
Newala.
SHERIA
NA KANUNI ZA UTEKELEZAJI
Kila mmiliki wa chombo cha
kusafirisha abiria kwa kutumia Bodaboda na Bajaji ni wajibu chombo chake
kukilipia Leseni ya Usafirishaji. Kutakuwa na msako mkali kwa waendesha
pikipiki na Bajaji ambao utashirikisha Maafisa wa SUMATRA na Jeshi la polisi
ili kuwabaini wote ambao watakuwa wanakeuka sheria hii na kanuni za
usafirishaji wa abiria kwa kutumia Pikipiki na Bajaji/ Guta kukamatwa na
kufikishwa mahakamani.
Tunatoa wito kwa wamiliki
wote wa vyombo vya usafirishaji (Pikipiki, Bajaji na Guta) kuvikatia haraka
Leseni vyombo vyenu ili kuepukana na usumbufu pindi operesheni ya kudumu ya
ukaguzi wa vyombo hivyo.
CHINI
YA KIFUNGU 5A CHA SHERIA YA SUMATRA NA. 9 YA 2001
Masharti ya leseni za
pikipiki kwa mujibu wa Kanuni namba 13,14 na 15 ya Kanuni za Leseni ya Usafirishaji
kwa kutumia Pikipiki yatamhitaji mmiliki wa leseni kuhakikisha kwamba:
1.
Pikipiki ya abiria inakuwa katika hali ya
usalama na ubora
2.
Derive wa pikipiki ana leseni inayomruhusu
kuendesha pikipiki husika
3.
Pikipiki ya magurudumu mawili haibebi zaidi ya
abiria mmoja
4.
Dereva wa pikipiki anavaa sare safi na
nadhifu na abandike kitambulisho mahali kinapoweza kuonekana na mtu yoyote
5.
Dereva wa pikipiki azingatie vikomo vya kasi
ya mwendo uliowekwa
6.
Dereva wa pikipiki ya abiria avae kofia
ngumu (Helmet) yenye namba ya utambulisho wakati wote anapoendesha pikipiki
7.
Dereva wa pikipiki ahakikishe kuwa abiria
wake amevaa kofia ngumu wakati wote wa safari
8.
Dereva wa pikipiki haruhusiwi kutumia simu
ya mkononi wakati wote anapoendesha
9.
Dereva wa pikipiki za magurudumu mawili
haruhusiwi kubeba abiria mwenye umri chini ya miaka tisa (9)
10.
Dereva wa pikipiki akiwa kazini asifanye
vitendo vifuatavyo
a) Kutumia
lugha ya uhasama au matusi kwa abiria
b) Kuendesha
pikipiki akiwa amekunywa pombe au kutumia madawa ya kulevya
c) Kuendesha
pikipiki kwa uzembe au namna ya hatari au kinyume na sheria ya usalama
barabarani na sheria zingine.
Kwa
maelezo zaidi fika katika ofisi ya Mkurugenzi wa Mji Masasi.
Clarence
Chilumba,
Ofisa
Habari Halmashauri ya Mji
MASASI.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD