TANGAZO
Na Boppe Kyungu,Mkuranga.
Mbunge wa jimbo la Mkuranga mkoani Pwani Abdallah Ulega amewataka
wananchi wa jimbo hilo kuwa na utamaduni
wa kufanya kazi za uzalishaji mali kwa lengo la kujiongezea kipato ili kuendana
na kauli mbiu ya Rais Magufuli ya “Hapa kazi tu”.
Aliyasema hayo jana wakati wa ziara yake ya kuwashukuru wananchi wa jimbo la Mkuranga kwa
kumchagua na kuwa mbunge wao sambamba na kura nyingi walizopga zilizompa
ushindi Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli.
Ziara hiyo ilifanyika kwenye kijiji cha Mkuranga eneo la
Godown kata ya Mkuranga ambayo pia iliambatana
na uoneshaji wa shughuli za vikundi vya ujasiliamali vilivyopo katika Kata ya
Mkuranga.
Alisema ana imani kubwa na wananchi wa jimbo hilo ambao kwa umoja wao wamefanya
kazi kubwa kwa kukichagua chama cha mapinduzi na kwamba muda wa siasa umeisha kilichobaki
kwa ni ya kuwatumikia, kuwatetea na
kuwasemea wananchi wa jimbo la Mkuranga ili kuleta maendeleo.
Alisema amefurahishwa na namna vikundi vya akinamama,
vijana na wazee wanavyojishughulisha na ujasiliamali ili kujiongezea kipato
huku akitoa sharti kuwa yuko tayari kusaidia vikundi vya wajasiliamali endapo
ataona kazi wanazozifanya.
“Niko tayari kutoa msaada kwa vikundi vyote vya
wakulima,wafugaji na wafanyabiashara…lakini ni lazima nitembelee mradi husika
kwa lengo la kuhakikisha kwamba fedha nitakazotoa kwa ajili ya wajasiliamali
zinatumika kama ilivyokusudiwa na si vinginevyo”.alisema Ulega.
Kwa mujibu wa mbunge huyo alisema kuwa kwa vile vikundi
ambavyo hadi havina shughuli yoyote ya kufanya ni vyema wakaanza kujiandaa ili siku atakapotembelea eneo husika akute shughuli hiyo ipo na inaendelea
kufanya kazi.
Alisema lengo ni
kufanya vikundi vyote vya ujasiliamali vilivyopo jimbo la Mkuranga kusonga
mbele hatimae wananchi wa jimbo hilo wawe na maisha bora na kuachana na dhana
ya kuwa omba omba kila siku.
Alisema kwa kutumia nafasi aliyonayo yuko tayari kutafuta masoko ya bidhaa zao ili bidhaa hizo
ziuzwe na hatimae wanufaike na miradi ambayo wameianzisha.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD