TANGAZO
Na Clarence Chilumba,Nachingwea.
Vikundi vya uzalishaji mali wilayani Nachingwea mkoani Lindi
vimeziomba Taasisi za kifedha zinazotoa mikopo nchini kuangalia upya riba
zinazotozwa ili viweze kunufaika na mikopo inayotolewa na taasisi hizo na
kukuza mtaji.
Wakizungumza wakati wa mafunzo ya ujasiliamali yaliyoshirikisha
vikundi vya Kata ya Kilimanihewa yaliyoandaliwa na Diwani wa kata hiyo,
Michinge Mchopa baadhi ya wanachama wa vikundi hivyo walisema riba kubwa
zinazotozwa na taasisi hizo zimekuwa ni kikwazo kwa vikundi vingi
hasa vya vijijini kuweza kukopa kwani wanakuwa na hofu ya kushindwa
kurejesha kwa wakati.
Mariam Mohamed mwenyekiti wa kikundi cha Tuyangatane
kinachojishughulisha na ufugaji wa kuku wa kienyeji alisema kuwa vikundi vingi
vinashindwa kuendelea kutokana na kukosa mitaji ya kutosha kwani wamekuwakichangishana
kiasi kidogo cha fedha na kuanzisha miradi lakini vinashindwa kunufaika na
taasisi hizo kutokana na tozo kubwa la riba na urasimu katika upatikanaji wa
mikopo hivyo taasisi hizo kuwanufaisha watu binafsi badala ya vikundi.
Alisema kuwa wananchi hasa wanawake wamehamasika kuanzisha vikundi
kwa lengo la kuanzisha miradi ambayo itanalenga kumkomboa mwanamke kuachana na
utegemezi ila kikwazo ni riba ambayo pia inasababishwa na kutokuwa na taasisi
nyingi zinazotoa mikopo katika wilaya ya Nachingwea.
“Tatizo hili kwa kiasi kikubwa linachangiwa na kutokuwa na taasisi
nyingi zinazotoa mikopo kwa vikundi kama vyetu hapa wilayani kwetu”alisema
Mariam.
Naye mjumbe wa kikundi cha Nguvukazi kinachojishughulisha na
ubanguaji wa korosho alisema kuwa kama kikundi hicho kingekuwa na mtaji wa
kutosha wangeweza kununua korosho za kutosha kubangua mwaka mzima tofauti na
ilivyo hivi sasa ambapo ubaguaji unasuasua kwani inawalazimu kuuza kwanza kiasi
kidogo cha korosho wanazozibangia ndipo waangaike kutafuta korosho jambo mbalo
linaatahari kwani muda wa kununua korosho zisizobanguliwa ukipita uwa
hazipatikani tena.
Diwani wa kata hiyo Michinge Mchopa aliwaasa wanavikundi
hao kuhakikisha wanaboresha utawala wa vikundi vyao na kufungua akaunti kwenye
taasisi za kifedha zilizopo ili kurahisisha katika upatikanaji wa mikopo.
Alitaja mambo mengine ya kuzingatia ni kuhakikisha kikundi inakuwa
na katiba mbayo ndiyo itakuwa ni mwongozo na sheria kuu na ndio itasaidia
katika uendeshaji na udhibiti wa nidhamu ya wanakikundi.
Katika mafunzo hayo ya ujasiliamali vikundi 46 vya kata ya
Kilimanihewa vilijengewa uwezo na benki ya NMB ya namna ya kuanzisha miradi na
utunzaji wa kumbukumbu za kifedha na umuhimu wa kuweka akiba kwenye
taasisi za kifedha kuwa ni pamoja na kujenga mahusiano mazuri na taasisi hizo
hivyo kurahisisha katika upatikanaji wa mikopo pindi kikundi kinapoamua kukopa.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD