TANGAZO
Diwani wa kata ya Mkuti Halmashauri ya mji wa Masasi Hamza Machuma.
Na
Hamis Nasiri, Masasi.
DIWANI
wa kata ya Mkuti jimbo la Masasi, Hamza Machuma amenunua vifaa vya kujifungulia
akinamama wajawazito vyenye thamani ya shilingi milioni 2.3 ambapo kila mjazito
ambaye yupo katika kata hiyo atapatiwa seti moja bure pindi anapokwenda hospitalini
Kwa ajili kujifungua.
Diwani huyo ameamua kununua vifaa hivyo kwa
fedha zake za mfukoni kwa lengo la kuwaondolea adha akinamama wajawazito ambapo
wanapokwenda katika hospitali ya mji Masasi Mkomaindo akinamama hao hutakiwa
kubeba vifaa vya kujingulia kutokana na hospitali hiyo kukabiliwa na changamoto
ya ukosefu wa vifaa mbalimbali vya kujingulia wajawazito.
Akizungumza na Blog ya Mtazamo mpya jana
katika ofisi ya serikali ya mtaa wa Mkuti mara baada ya kukabidhi seti mbili ya
vifaa hivyo kwa akinamama wajawazito wawili ambao ndio wa kwanza kuanza
kunufaika na mpango huo Machuma alisema vifaa hivyo atakuwa akitoa bure.
Alisema
kuwa kutokana na kero ya akinamama wajawazito wanayoipata katika hospitali ya
Mkomaindo ya kuelezwa kila anayekwenda kujifungua anatakiwa kununua vifaa vya
kujifungulia kwa gharama yake mwenyewe jambo ambalo wajawazito wengi
walililalamika kwa kwa kuwa baadhi yao hawawezi kumudu gharama za vifaa hivyo
Machuma
alisema kwa vifaa vya awamu ya kwanza alivyonunua vinathamani ya sh.2.3 milioni
na kwamba hata kama kila siku watakuwa wakijitokeza wajawazito 10 au 12 wa kata
hiyo kwenda kuchukua seti moja kwa kila mjamzito bado vitakuwepo na kwamba
vitakuwa vikitolewa katika ofisi ya serikali ya Mtaa wa mkuti kwa muda wa kazi.
“Nimeguswa na tatizo la wajawazito
wanapokwenda pale hospitali na kuelezwa kuwa hakuna vifaa vya kujifungulia na
kutakiwa wakanunue wenyewe ndio maana nimeamua kununua kwa ajili ya wajawazito
wa kata yangu na nitafanya hivi kwa kipindi chote cha uongozi wangu ndani ya miaka
mitano,”alisema Machuma
Machuma
alivitaja baadhi ya vifaa hivyo kuwa nyembe,mikasi,groves za kuvaa mikokoni
,beseni za kuwekea maji pamoja na nailoni ngumu ambazo mama mjamzito hutandika
wakati anapojiandaa kujifungua,aidha diwani ameendesha zoezi la kuua wadudu
wanaotambaa na kuruka bure katika kila nyumba iliyopo katika kata yake ili
kukabiliana na magonjwa yanoyoweza kuambikizwa na wadudu hao.
Kwa upande wake Shakira Saidi mkazi wa mtaa wa
Robeni katika kata hiyo ya Mkuti alisema ameshukuru kupata seti moja ya vifaa
hivyo kwani hivi sasa yupo karibu kujifungua na hivi anatarajia kwenda
hospitali kujifungua hivyo kupata msaada huo kwake ni jambo la faraja.
Naye Kuruthumu Afla mkazi wa mtaa wa Mkuti
alimshukuru diwani huyo kwa kuliona tatizo hilo kwa wajawazito ambalo kwa muda
mrefu wamekuwa wakikabiliana nalo wanapokwenda hospitalini na sasa adha hiyo
itakwisha kwa akinamama wa kata ya Mkuti.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD