TANGAZO
Clarence Chilumba, Masasi
Wakazi wawili wa wilaya ya Masasi
mkoani Mtwara wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 kila mmoja kwa makosa ya kubaka
watoto wadogo wenye umri chini ya miaka 18 kwa nyakati tofauti.
Hukumu hizo zote zilizovuta
hisia kwa wananchi wa wilaya ya Masasi zilitolewa kwa pamoja Desemba 31, 2015
katika mahakama ya wilaya ya Masasi mkoani Mtwara huku wananchi hao
wakiipongeza mahakama hiyo kwa kutenda haki katika maamuzi ya kesi za ubakaji.
Mbele ya hakimu Halfani
Ulaya mwendesha mashtaka Suleyman Omari
alidai washtakiwa walitenda makosa hayo kwa nyakati tofauti katika
vijiji vya Chakama halmashauri ya mji wa Masasi pamoja na kijiji cha Mkalapa
halmashauri ya wilaya ya Masasi mkoani Mtwara.
AKitoa hukumu hizo alhamisi
ya Desemba 31,2015 Hakimu wa mahakama ya wilaya ya Masasi Halfani Ulaya alisema
watuhumiwa hao walitenda makosa hayo ya
ubakaji mwaka jana kwa nyakati tofauti tena kwa makusudi huku wakijua ni kosa la jinai na
ukiukwaji wa maadili ya kitanzania.
Waliohukumiwa kwenda jela ni
pamoja na Yusufu Sadiki Baharia (51) mkazi wa kijiji cha Chakama Halmashauri ya
mji wa Masasi ambaye mnamo April 4, 2015 huko katika kijiji cha Chakama majira
ya saa 9:00 jioni alimbaka mtoto mwenye umri wa miaka 9 (jina linahifadhiwa)
aliyekuwa anasoma darasa la tatu katika shule ya msingi Chakama.
Alidai kuwa Yusufu
alitekeleza unyama huo eneo la shamba la mzee Rupu kijijini hapo kwa kumbaka
mtoto huyo na kumsababishia majeraha makubwa yaliyothibitishwa na daktari wa
hospitali ya Mkomaindo mjini Masasi Patrick Chikumba April 4, 2015.
Mwingine aliyehukumiwa
kifungo cha miaka 30 jela ni David Selemani (20) mkazi wa kijiji cha Mkalapa
halmashauri ya wilaya ya Masasi ambaye alitenda kosa hilo Novemba 2013, majira
ya saa 12:00 jioni huko katika kijiji cha Mkalapa.
Kwa mujibu wa Hakimu Ulaya
alisema ameridhishwa na upande wa utetezi ulioletwa na mashahidi wanane mahakamani hapo na kwamba uamuzi huo ni wa haki na kisheria kwani walitenda makosa
hayo ya ubakaji huku wakijua kuwa ni makosa
ya jinai.
Washtakiwa hao walipotakiwa
kujitetea hawakusema chochote na kwamba wote wamekiri kuwa kwa makusudi
walitenda makosa hayo huku mahakama ikitoa onyo kali kwa watakaobainika
kuendelea na vitendo hivyo vya kinyama na kikatili dhidi ya watoto.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD