TANGAZO
Na Bashiru Kauchumbe,Ruangwa.
Jumla ya kaya 64 katika kijiji cha Mtondo wilaya ya Ruangwa mkoani
Lindi hazina mahali pa kuishi baada ya
nyumba zao kuezuliwa kwa upepo mkali ulioambatana na mvua.
Pia katika tukio hilo la kusikitisha jengo la zahanati katika kijiji
hicho liliezuliwa kwa upepo huo mazingira yaliyosababisha kusimama kwa huduma
za afya kwa wananchi kijijini hapo.
Akisimulia mkasa huo kwa waandishi wa habari, Diwani wa Kata ya
Nambilanje Adala Chigope alisema kuwa tukio
hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita majira ya saa 1:00 usiku .
Alisema upepo huo mkali ulioambatana na mvua
kubwa iliyonyesha kijijini hapo imeleta athari kubwa kutokana na baadhi ya
miundombinu ikiwemo barabara kuharibika vibaya.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Ruangwa Mariam Mtima aliyeambatana na wajumbe wa kamati ya Ulinzi na usalama na wa
kamati ya maafa wilayani humo aliuagiza uongozi wa serikali ya kijiji kufanya
tathimini ka kumpelekea taarifa kwa ajili ya utekelezaji.
Alisema tukio hilo ni la kusikitisha na kwamba yeye kama mwenyekiti wa
kamati ya maafa ya wilaya alifikia kijijini hapo kwa lengo la kuangalia hali
halisi ya maafa hayo pamoja na kuwafariji waathirika.
“Nawaagiza uongozi wa kijiji pamoja na kata… kufanya tathimini ili
kupata takwimu halisi za waathirika pamoja na mali zao ili nasi tuweze kutoa
taarifa Ofisi ya Waziri Mkuu kitengo cha maafa.
Kwa mujibu wa mkuu huyo wa wilaya aliwaondoa hofu wananchi wote
walioathirika na mvua hizo na kwamba serikali iko pamoja nao huku akitoa rai
kwa wananchi walionusurika kwenye tukio hilo kuwasaidia wenzao.
Ofisa Mtendaji wa Kata ya Nambilanje
Abdala Tamba alisema kwa sasa kaya zilizoathirika
zinatunzwa na ndugu na jamaa wakati wanasubiri msaada kutoka serikalini.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD