TANGAZO
Mbunge wa Jimbo la Nachingwea mkoani Lindi Hassan Masala.
Christopher Lilai,Nachingwea.
Mbunge wa
jimbo la Nachingwea,Hasani Masala ametoa pikipiki tatu zenye thamani ya
shilingi milioni sita na fedha taslimu shilingi laki tano kwa Umoja
wa madereva wa bodaboda wilayani hapa huku akiwataka kusajili umoja huo ili
utambulike kisheria.
Mchango
huo ameutoa alipokutana na madereva wa bodaboda siku ya jumamosi mwishoni mwa
wiki iliyopita kwenye ukumbi wa Nachingwea Resort ambapo licha ya kusikiliza
kero mbalimbali wanazokutananazo aliwahasa kuunda umoja wenye nguvu na kuwa na
mfuko wa kuweka na kukopa ili uwasaidie katika kuwapatia mitaji.
Aliwataka
viongozi wa umoja huo kuwatambua madereva wote wa bodaboda wilayani na kwa
kupitia vituo vyao vya kazi maarufu migundi kuunda uongozi ambao ndio utakuwa
ndio wawakilishi wa kila mgundi hivyo kurahisisha mawasiliano kati ya uongozi
na taasisi mbalimbali ikiwemo jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani.
Masala
alisema kuwa msaada wa pikipiki alizowapatia ni mtaji katika kuanzisha
VICCOBA endelevu ambapo ndio patakuwa kimbilio kwa madereva hao ili kuachana na
kutumwa na badala yake waweze kumiliki pikipiki zao wenyewe kwa kukopeshana
wenyewe kupitia mfuko huo.
“Mimi
nipo nyuma yenu katika kuhakikisha mnafanikiwa kuunda mfuko wa
Viccoba endelevu ambacho ndicho chombo pekee kitakachokuwa mkombozi
wenu”alisema Masala.
Aliwahasa
madereva hao wa bodaboda kuacha kutumiwa vibaya na wanasiasa kwani muda wa
siasa umepita badala yake waendelee na majukumu yao ya kujitafutia kipato na
serikali ipo nyuma yao na iwapo kuna tatizo ofisi yake ipo wazi kupokea
malalamiko yao.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD