TANGAZO
Christopher Lilai,Nachingwea.
Wakati
shule za msingi nchini zinatarajiwa kufunguliwa hivi karibuni, Mkurugenzi
mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Nachingwea,Injinia Jackson Masaka
amewaonya walimu wa wakuu wa shule za msingi kutotoza michango ambayo
imekataliwa na kuzingatia maagizo ya serikali juu ya utozaji wa michango.
Masaka
alitoa onyo hilo siku ya ijumaa kwenye ukumbi wa chuo cha ualimu Nachingwea
wakati anafungua mkutano wa kazi wa waratibu wa elimu wa kata na walimu wakuu
wa shule za msingi ambapo alisema kuwa wakati miongozo ya serikali
inaendelea kutafsiriwa juu ya michango ni vyema wakasitisha kabisa kuchangisha
pesa wakati huu wa usajili wa wanafunzi wa darasa la kwanza.
Hata
hivyo alibainisha kuwa iwapo shule itaona kuna haja ya kuwa na michango kwa
ajili ya kuboresha mazingira ya utoaji wa elimu ikiwemo ujenzi wa vyumba vya
madarasa na utengenezaji wa madawati ni lazima jamii ikashirikishwa kupitia
uongozi wa serikali ya kijiji na kukubaliwa na wananchi
wote.
“Kama
kuna haja ya kuwa na michango ni lazima muishirikishe serikali ya kijiji kwani
ndio wenye shule yao ili taratibu za kuishirikisha jamii zifanyike ninyi mna
jukumu la kuwahamasisha juu ya umuhimu wa mchango husika” alisema
Injinia Masaka.
Akizungumzia
nidhamu ya walimu,Mkurugezi huyo aliwataka kufanya kazi kwa kuzingatia taratibu
za utumishi wa umma ikiwemo kuwemo kwenye kituo cha kazi na kuingia darasani
kwani zipo tabia ya baadhi ya walimu kujihusisha na ulevi muda wa kazi na kuwa
hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa kwa yeyote atakayepatikana na tabia hizo.
“Kuna
walimu wanaliangusha Taifa kwa kuwa na vitendo vya utoro na ulevi,
ki ukweli naahidi kuwachukulia hatua walimu hao wasipojirekebisha”Alisema
Masaka.
Akimkaribisha
mkurugenzi huyo,Ofisa elimu msingi wa halmashauri hiyo,Makwasa Bulenga
alibainisha kuwa licha ya wilaya hiyo kushuka hadi nafasi ya nne
kimkoa mwaka jana kwenye matokeo ya darasa la saba toka nafasi ya
kwanza mwaka juzi hali ya ufaulu imeongeeka na kufikia asilimia 59 kwa jana toka
asilimia 43 mwaka juzi.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD