TANGAZO
MAMLAKA ya Mapato (TRA)
imeshakusanya Sh bilioni 11.9 kutoka kwa wafanyabiashara waliokuwa wamekwepa
kulipa kodi. Kiasi hicho ni sehemu ya Sh bilioni 80 zinazotakiwa kukusanywa
kutoka kwa wafanyabiashara hao wanaodaiwa waliondosha kontena katika bandari za
nchi kavu kinyume cha taratibu za forodha.
Hata hivyo, kampuni 19
za wafanyabiashara hao waliopewa siku saba na Rais John Magufuli wawe wamelipa
kodi baada ya kubainika kuhusika kukwepa kodi katika sakata la utoroshaji wa
kontena 329 kutoka katika baadhi ya bandari kavu, hawajalipa kodi hiyo wakidaiwa
kugoma kulipa adhabu.
Hayo yalielezwa jana
jijini Dar es Salaam Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata katika mkutano
na waandishi wa habari ambako pia alisema mamlaka imevunja rekodi ya ukusanyaji
kodi baada ya kukusanya Sh trilioni 1.4 Desemba mwaka jana kutoka Sh trilioni
1.3 za Novemba 2015.
Waliogomea adhabu “Hizi
kampuni zingine 19 sio kwamba wamegoma kulipa kodi, ila wameomba wafanye
reconciliation (mlinganisho) ya miamala na TRA kuhusu kiasi ambacho wanatakiwa
kulipa. Wanachogomea kulipa ni zile adhabu ambazo wanatakiwa kuzilipa kwa
kukwepa kodi,” alisema Kidata.
Kidata alisema Sh
bilioni 80 zinatakiwa kulipwa na wafanyabiashara hao ambao waliondosha kontena
katika bandari za nchi kavu bila kulipa ushuru. Siku ya mwisho ambayo iliwekwa
na Rais Magufuli ilikuwa Desemba 12.
Baada ya kubainika
kuwepo kwa upotevu huo, TRA iliwaandikia hati ya malipo inayowataka
wafanyabiashara hao kulipa kodi stahiki pamoja na adhabu. Baadhi ya
wafanyabiashara wanadai kuwa walishalipa kodi hiyo kupitia kwa mawakala ambao
baadhi yao wametoroka hivyo kuwataka walipe adhabu ni kuwaonea.
Wavuka rekodi Katika
hatua nyingine, TRA imevunja rekodi ya ukusanyaji wa kodi baada ya kukusanya Sh
trilioni 1.4 Desemba mwaka jana kutoka Sh triKidata alisema katika kipindi cha
Julai hadi Desemba, mamlaka yake imekusanya Sh trilioni 6.4 ikilinganishwa na
lengo ambalo lilikuwa ni kukusanya Sh trilioni 6.6 ambazo ni sawa na asilimia
95.5 ya makusanyo yote.
Kidata alisema
kuongezeka kwa makusanyo ya kodi katika kipindi hiki kunatokana na mikakati
madhubuti ambayo TRA imeiweka tangu Serikali ya awamu ya tano iingie madarakani
.
Akizungumzia usajili wa
pikipiki ambao uliisha Desemba 31, 2015, Kidata alisema TRA imeongeza muda wa
mwezi mmoja kutoa fursa kwa ambao hawajakamilisha usajili huo wafanye hivyo.
Alisema TRA imechukua uamuzi huo kwa kuwa usajili huo ulikumbwa na changamoto
kadhaa ambazo zilisababisha usajili kutokamilika kwa asilimia 100.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD