TANGAZO
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Masasi mkoani Mtwara Fortunatus Mathew Kagoro akizungumza wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani.
Na Clarence Chilumba,Masasi.
MKURUGENZI wa Halmashauri ya mji Masasi mkoani Mtwara Fortunatus
Kagoro amewaondoa hofu madiwani wa halmashauri hiyo kuhusu utekelezaji wa
shughuli za maendeleo katika kuwahudimia wananchi.
Kagoro ameyasema hayo leo wakati wa kikao cha baraza la madiwani
kilichofanyika katika ukumbi wa karakana ya maji mjini hapa.
Alisema atahakikisha kuwa anashirikiana bega kwa bega na
madiwani wa halmashauri katika kufanya utekelezaji wa shughuli za maendeleo ili
kuweza kuwahudumia wananchi hatimaye kuifanya Masasi kuwa nuru ya maendeleo
wilayani humo.
Kagoro alisema anaamini watendaji wake katika halmashauri hiyo
hawatafanya kazi kwa kuangalia itikadi za vyama bali watakuwa na ushirikiano
mzuri na madiwani hao kutimiza malengo ya halmashauri.
Aliongeza kuwa atahakikisha suala la mapato linakusanywa vema na
halmashauri kwa kushirikiana na madiwani hao pamoja na watendaji wake ili
kuweza kuwa na mapato ya kutosha
yatakayoifanya iweze kutoa huduma kwa wananchi.
“Ondoeni hofu madiwani mimi nitafanya kazi na nyinyi kwa
kushirikiana pamoja ili halmashauri yetu tupate maendeleo kwa kasi nakushukurui
sana tangu tumeanza tunashirikiana vizuri,”alisema Kagoro.
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Sospeter Nachunga
alisema ushirikiano ni jambo jema kati ya madiwani na watendaji na kwamba hatua
hiyo itasaidia kuifanya halmashauri kuwa na maendeleo.
Alisema madiwani wanapaswa kuweka kando itikadi za vyama vyao
badala yake wafanye kazi kwa kuangalia maslahi ya Masasi.
“Nashukuru tangu nianze kuongoza halmashauri hii sijaona mpasuko
baina ya madiwani na hata kwa upande watendaji tunafanya kazi vizuri na
kushirikiana na nawapongeza sana kwa hili,”alisema Nachunga
Alisema bila kuwa na ushirikiano kati ya watendaji wa ofisi ya
mkurugenzi na madiwani itakuwa vigumu kupata maendeleo ambayo kila mara
wamekuwa wakikaa vikao kwa ajili ya kujadili hivyo nguvu ya pamoja ndio nyenzo
ya maendeleo.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD