TANGAZO
Kaimu Meneja wa NHIF mkoa wa Mtwara Dk.Leonard Miti (kushoto) akimkabidhi msaada wa mashuka 500 mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Masasi Mheshimiwa Sospeter Nachunga hii leo katika viwanja vya Hospitali ya Mkomaindo mjini Masasi.
Na Clarence Chilumba,Masasi
TC.
Mfuko wa Taifa wa Bima ya
afya (NHIF) mkoa wa Mtwara umetoa msaada wa mashuka 500 kwa hospitali ya
Mkomaindo Halmashauri ya mji wa Masasi kwa lengo la kukabiliana na tatizo la
mashuka lililokuwa likiikabili hospitali hiyo kwa muda mrefu.
Msaada huo umekuja kufuatia
agizo alilolitoa Naibu waziri TAMISEMI anayeshughulikia Utawala Bora na
Utumishi Mhe: Selemani Jafo alipofanya ziara hospitalini hapo mwishoni mwa wiki
iliyopita ambapo aliuagiza uongozi wa bodi ya hospitali hiyo kwa kushirikiana
na ofisi ya mkurugenzi kulitafutia ufumbuzi tatizo la mashuka hospitalini hapo.
Akisoma taarifa kwa mgeni
rasmi leo wakati wa makabidhiano ya msaada huo mganga mfawidhi wa hospitali ya
Mkomaindo Dk.Selijo alisema hospitali
hiyo inayomilikiwa na serikali ina uwezo wa kuhudumia wagonjwa wapya wa nje (OPD)
150 kwa siku.
Alisema hospitali hiyo ina
upungufu mkubwa wa vitanda na mashuka ukilinganisha na mahitaji ambapo pamoja
na mapungufu hayo uongozi wa hospitali hiyo kwa kushirikiana na mashirika
mbalimbali ya serikali na yasiyo ya kiserikali umekuwa ukifanya jitihada za
kukabiliana na changamoto hizo ambazo zinaathiri kwa kiasi kikubwa utoaji wa
huduma za afya katika hospitali hiyo.
“Ndugu mgeni rasmi tumekuwa
tukifanya jitihada mbalimbali za kukabiliana na hali hii…ambapo kutokana na
ushawishi huo tumefanikiwa kupokea msaada wa mashuka 121 kutoka kwa Benki ya
CRDB iliyotoa mashuka 62, Mfuko wa Bima ya afya mashuka 19 na mbunge wa jimbo
la Masasi aliyetoa mashuka 40”alisema Dk Selijo.
Kwa mujibu wa mganga
mfawidhi wa hospitali ya Mkomaindo alisema idara ya afya katika bajeti yake ya
mwaka 2015/2016 imepanga kununua mashuka 245 kupitia fedha za mfuko wa pamoja
wa sekta ya afya nchini ili kuondoa kabisa suala na upungufu wa mashuka.
Kwa upande wake kaimu
meneja wa mfuko wa Taifa wa Bima ya afya mkoa wa Mtwara Dk.Leonard Miti alisema
wametoa msaada wa mashuka hayo kwa lengo la kuendeleza mahusiano yaliyopo
katika ya NHIF na hospitali hiyo ambayo kila mwezi NHIF huilipa zaidi ya
shilingi Milioni 10.
Alisema msaada huo umepunguza
kero ya mshuka kwa wagonjwa katika hospitali hiyo na kwamba menejimenti ya
hospitali hiyo kwa sasa ni vyema wakakaa chini kuona ni kwa jinsi gani wanaweza
kupata mkopo wa ukarabati na uboreshaji wa majengo pamoja na mkopo wa ununuzi
wa vifaa tiba.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD