TANGAZO
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkomaindo Halmashauri ya mji wa Masasi Dkt.Gaspar Kumalija akisoma taarifa mbele ya naibu Waziri ofisi ya Rais TAMISEMI Utawala Bora na Utumishi Mh: Selemani Jafo (hayuko pichani) hii leo katika hospitali hiyo alipofanya ziara.
Na Clarence
Chilumba,Masasi.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI-Utawala Bora na Utumishi Selemani Jafo ameimwagia sifa Lukuki Hospitali ya Mkomaindo Halmashauri ya Mji wa Masasi kwa kutoa huduma bora za chanjo kwa watoto na wanawake walio katika umri wa kubeba mimba.
Pongezi hizo zimekuja baada ya Hospitali hiyo kufikia kiwango cha ufanisi cha utoaji wa huduma za chanjo kwa asilimia 95.6 kwa mwaka 2015 kutoka asilimia 80 kwa mwaka 2014 kwa chanjo ya DPTHB3 ambayo ndio kipimo cha ufanisi wa huduma za chanjo inayotumika nchini.
Akizungumza wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa maeneo mbalimbali katika
utekelezaji wa sera ya “HAPA KAZI TU” alisema kiwango walichokionesha katika
utoaji wa huduma za chanjo kinapaswa kuiga na hospitali zingine nchini na
kwamba serikali iko tayari kuisaidia hospitali hiyo ya Mkomaindo katika kuleta
vifaa mbalimbali ikiwemo nishati ya gesi kwa ajili ya kuendeshea majokofu ya
kuhifadhia chanjo hizo.
Akisoma taarifa ya idara ya afya halmashauri ya mji wa Masasi mganga
mkuu wa hospitali ya Mkomaindo Dk.Gaspar Kumalija alizitaja baadhi ya
changamoto zinazoikabili hospitali hiyo ikiwemo upungufu wa watoa huduma wenye
ujuzi,ucheleweshaji wa fedha za mfuko wa pamoja wa sekta ya afya pamoja na
upungufu wa magari na uchakavu wa magari yaliyopo.
Pia uchakavu wa miondombinu katika vituo vya kutolea huduma za afya na
uhaba wa vituo vya kutolea huduma za afya vya serikali katika baadhi ya maeneo
hasa yale yaliyopo pembezoni mwa mji katika kata za Matawale,Temeke na Marika
ni changamoto zingine zinazoikabali hospitali hiyo ya halmashauri ya mji wa
Masasi.
Kwa mujibu wa Dk.Kumalija aliiomba serikali kupitia wizara ya afya
kuajiri watumishi wa sekta ya afya wenye ujuzi wa kutosha ili kukabilana na
upungufu wa watumishi pamoja na serikali kuleta magari na vifaa tiba
hospitalini hapo.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD