TANGAZO
Moja ya Mabanda ya Nguruwe (picha ya maktaba)
JAMHURI YA MUUNGANO
WA TANZANIA
OFISI YA RAIS TAWALA
ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
OFISI YA MKUU WA
MKOA WA MWANZA
TAARIFA KWA UMMA.
YAH: MLIPUKO WA
UGONJWA WA HOMA YA NGURUWE
Kumetokea mlipuko wa ugonjwa wa Homa ya
Nguruwe (African Swine Fever) Wilaya ya Nyamagana, Kata za Mabatini, Mirongo
kishiri na Buhongwa na Igoma. Mlipuko huu umedhibitishwa kwa uchunguzi
uliofanyawa na Maabara ya Chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA)
Ugonjwa wa Homa ya Nguruwe unasababishwa na
Virusi (African Swine fever virus). Madhara yake ni makubwa kwa wafugaji na
kiuchumi kwani husababisha vifo asilimia 100 (100%) kwa Nguruwe wote
walioambukizwa.
Ugonjwa wa Homa ya Nguruwe hauna chanjo
wala tiba na hauambukizi Binadamu. Njia pekee ya kudhibiti ugonjwa huu ni
kuzuia kueneoa kwa maambuzi toka eneo lenye maambukizi kwenda eneo
lisiloambukizwa.
HATUA ZA
TAHADHARI KUZUIA KUENEA KWA UGONJWA WA HOMA YA NGURUWE
·Wafugaji
waepuke kununua Nguruwe kutoka kwenye Maeneo/Mashamba yenye ugonjwa
·Nguruwe
wafugwe kwenye Mabanda imara na waepuke kutembea ovyo
·Nguruwe
wasilishwe mizoga au masalio ya chakula kutoka vyanzo visivyojulikana
·Teketeza
Mizoga iliyokufa kwa ugonjwa na ufanye usafi kwa kuzingatia maelekezo ya
watalaam na kwa kutumia dawa za kuua vimelea vya magonjwa (disinfectants)
·Wakulima
watoe taarifa ya uwepo wa ugojwa haraka kwa mtalaa wa Mifugo aliye karibu
·Wananchi
wazingatie maelekzo yote yanaotolewa pindi watalaam wa Mifugo wanapoweka
Tangazo la Karantini (QUARANTINE) la kuzuka kwa ugonjwa wa
Homa ya Nguruwe.
IMETOLEWA 11,DESEMBA,
2015.
Dkt Yohana D.
Sagenge
Kny: KATIBU TAWALA
(M)
MWANZA
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD