TANGAZO
Maduka yaliyopo eeno la Maduka Tisa mjini Masasi wakiwa yamefungwa kupisha zoezi la usafi katika kutekeleza agizo la Rais Dk.John Pombe Magufuli.
Na Clarence
Chilumba,Masasi.
Wafanyabiashara wa maduka
na bidhaa mbalimbali mjini Masasi wamelazimika kufunga maduka yao kwa zaidi ya
masaa manne ili kupisha zoezi la usafi lenye lengo la kutekeleza agizo la Rais
Dk.John Pombe Magufuli la kuwataka watanzania kufanya usafi nchi nzima.
Agizo hilo lilitolewa na
Rais Dk.Magufuli kwa watanzania ili wananchi wote waweze kushiriki zoezi la
usafi siku ya tarehe 9,Desemba tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
Aidha baadhi ya wananchi wa
kata ya Jida walilazimika kufunga barabara kuu iendayo mkoani Mtwara mjini hapa
kwa muda katika eneo la Maduka Tisa huku wakiwataka abiria na watu binafsi
kushuka ili nao washiriki kwenye zoezi hilo muhimu lililoagizwa na Rais.
Wakizungumza kwa nyakati
tofauti baadhi ya wananchi mjini hapa wamepongeza uamuzi wa Rais wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania wa kubadilisha siku hiyo ya uhuru ya kufanya usafi badala
ya kushiriki kwenye shughuli za gwaride kama ilivyo kawaida kwenye viwanja vya
Uhuru.
Huko Ndanda nako wananchi
walilazimika kusimama kwenye vituo vya mabasi na kuwataka abiria kushuka ili
nao washiriki kwenye zoezi hilo muhimu kwa Taifa la Tanzania.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD