TANGAZO
Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakari Zuberi.
MUFTI wa Tanzania,
Shehe Mkuu Abubakari Zuberi amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Utawala wa Baraza
Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Karim Majaliwa kwa ajili ya kupisha
uchunguzi juu ya kashfa ya magari 82 pamoja na matumizi mabaya ya ofisi.
Katika
taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana, Mufti alisema
anatumia mamlaka aliyonayo kumsimamisha mkurugenzi huyo.
Hivi karibuni, Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA), iliijia juu Bakwata na kuitaka itoe maelezo ya
ongezeko la maombi ya msamaha wa kodi katika utoaji wa magari yanayopitishwa
katika taasisi hiyo ya dini, kutoka nje ya nchi.
Kwa
mujibu wa mamlaka hiyo, taasisi hiyo ya dini imekuwa na ongezeko kubwa la
maombi ya msamaha wa kodi kwa magari ya nje ambapo tangu mwaka 2006 hadi
Septemba mwaka huu, imeingiza magari 82 ya aina tofauti.
Katika
barua ya TRA kwa taasisi hiyo iliyosainiwa na Meneja Misamaha ya Kodi, Mwantumu
Salim ya Novemba 19, mwaka huu, ilibainisha kuwa kutokana na idadi kubwa ya
magari ya msamaha pamoja na maombi kuzidi kuongezeka, mamlaka hiyo imeamua
kuichunguza taasisi hiyo ili kujua magari hayo yanavyotumika.
Aidha,
TRA ilitoa siku saba kwa Bakwata iwasilishe kadi za usajili wa magari, kitabu
kinachoonesha safari za magari, stakabadhi za kulipia mafuta, bima, huduma za
matengenezo ya magari ikiwemo ushahidi wa maelezo na ushahidi kuhusu fedha
zilizotumika kununua magari hayo pamoja na hesabu za mwaka za taasisi.
TRA
ilifikia hatua hiyo baada ya Bakwata kuwasilisha maombi ya msamaha wa kodi kwa
TRA kwa ajili ya kuingiza nchini gari aina ya IVECO ambao hata hivyo msamaha
huo ulikataliwa hadi uchunguzi huo utakapokamilika.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD