TANGAZO
Askari wa kikosi cha jeshi la Magereza wilayani Masasi wakishiriki zoezi la usafi kwa kuchimba mtaro wa maji machafu uliopo kwenye eneo la magereza ya wilaya ya Masasi.
Baadhi ya wananchi wa kata ya JIDA Halmashauri ya mji wa Masasi wakifanya usafi kwenye eneo la maduka Tisa mjini humo hii leo ikiwa ni kutekeleza agizo la Rais Magufuli.
Wafanyabiashara wa eneo la KAUMU mjini Masasi wakifanya usafi hii leo.
Askari wa kikosi cha jeshi la polisi wilaya ya Masasi nao hawakuwa nyuma katika kutekeleza agizo la Amiri Jeshi mkuu wa majeshi ya Tanzania Rais John Pombe Magufuli.
Wananchi wakipakia uchafu kwenye gari tayari kwa kupeleka uchafu kwenye Dampo Kuu mjini Masasi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Masasi Fortunatus Mathew Kagoro (Kulia) akizungumza na Diwani wa kata ya Jida Mbwana A. Mkeng’endo (CUF) wakati wa zoezi la usafi hii leo mjini Masasi,mwenye baiskeli ni diwani wa kata ya Mkuti Hamza Katani Machuma.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Kambarage Halmashauri ya mji wa Masasi wakifanya usafi pamoja na walimu wao hii leo shuleni hapo.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD