TANGAZO
Na Bashiru Kauchumbe,Ruangwa.
Diwani wa kata ya
Mbekenyera Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa Rashid Hasani Nakumbya (CCM)
amependekezwa kuwa mgombea wa kiti cha Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya
Ruangwa mkoani Lindi kwenye uchaguzi utakaofanyika baadae mwezi huu.
Katika mchakato huo wa
uchaguzi uliokuwa na ushindani mkubwa kutoka kwa wagombea ndani ya chama cha
mapinduzi wilayani humo Nakumbya alipata
kura 10 na kuwabwaga vibaya wapinzani wake wa karibu
Andrew Chikongwe Diwani wa kata ya Nandagala aliyeambulia kura 6 pekee.
Wengine walioangushwa
na kada huyo maarufu katika siasa za Ruangwa ni Elius Nkane aliyepata kura 2 pamoja
na Rashidi Mnunduma aliyeambulia kura 1.
Aidha mtifuano mwingine
ulikuwa ni kwenye kinyang’anyiro cha kumpata mwana CCM atakayegombea nafasi ya
makamu mwenyekiti wa Halmashauri hiyo ambapo kwa pamoja wajumbe wa kikao hicho
walimpitisha kwa kauli moja diwani kijana wa kata ya Nanganga Shabani Kambona
aliyepata kura 12 na kumzidi mpinzani
wake Omari Songea diwani wa Kata ya Chibula aliyepata kura 7.
Wateuliwa hao kutoka ndani ya chama cha mapinduzi wilayani Ruangwa watapigiwa kura na wajumbe wa baraza la Madiwani katika mkutano wa uzinduzi wa baraza hilo Disemba 10,2015 kwa kukutanishwa na wagombea kutoka vyama vya CHADEMA pamoja na CUF.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD