TANGAZO
Na Clarence
Chilumba,Masasi.
Waumini wa Kanisa Katoliki
nchini wametakiwa wakati mwingine kutumia Lugha za makabila yao wakati
wanapofanya maombi binafsi wanapokuwa kanisani.
Wito huo umetolewa jana na
padre Mwajombe Mukasa wa kanisa katoliki kutoka shirika la Salvatorian- Migongo
Masasi wakati anatoa mahubiri kwa waumini wa kanisa hilo kigango cha Marika
jimbo la Tunduru Masasi mkoani Mtwara.
Alisema athari za kutotumia
lugha za makabila wakati wa maombi husababisha kupatikana kwa viongozi
wanaoutukuza uzungu na kuudharau utanzania.
Alisema kwa sasa waumini wa
kanisa hilo pamoja na makanisa mengine nchini wamegeuka na kuwa watumwa kifikra juu ya
matumizi ya lugha za asili katika maombi mbalimbali wawapo makanisani huku
wengi wakidhani kufanya maombi kwa kutumia lugha za asili ni dhambi kitu
ambacho sio sahihi kiimani.
Kwa mujibu wa padre huyo
alisema mara nyingi amekuwa akishangaa kwa waumini wa kanisa katoliki kushindwa
kuomba kwa kutumia lugha za makabila yao hasa wakati wa misa za kuombea wafu na
badala yake huishia kupamba maua kwenye makaburi.
“Inashangaza sana leo hii
kijana wa kitanzania hujisikia fahari kuzungumza lugha ya kiingereza…mara
kadhaa nimekuwa nikiwakumbusha waumini wa kanisa langu na hata makanisa mengine
kuwa mungu husikiliza zaidi maombi yanayoombwa kwa kutumia lugha ya asili ya
mama”alisema Mukasa.
Aidha katika mahubiri yake
aliwakumbusha waumini wa kanisa hilo kutambua kuwa familia ndio kitovu cha
imani ambapo aliwataka kutoa mafunzo ya kiroho kwa familia zao ili waweze
kupata familia zilizo bora.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD