TANGAZO
Baadhi ya nyumba zilizoathirika na mvua na upepo huo.
Na Christopher Lilai,Nachingwea.
Nyumba zipatazo 28 za wakazi wa kijiji cha
Namapwia,wilayani Nachingwea madarasa mawili na ofisi ya walimu wa shule ya
msingi yameezuliwa paa na upepo mkali uliombatana na mvua.
Akitoa maelezo ya tukio hilo kwa
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Nachingwea,Ahmadi Makoroganya
alietembelea kijiji hicho kujionea hali halisi, diwani wa kata hiyo Omari
Lingumbende,alisema kuwa upepo huo mkali ulitokea siku ya jumanne
wiki majira ya saa tisa alasiri ambapo licha ya uharibifu huo pia hekari 27 za
mashamba zimeathiriwa.
Diwani huyo ameiomba serikali kuchukua hatua ya
haraka kurekebisha madarasa hayo yaliyoezuliwa kwani gharama itakuwa kubwa
kwani hata kuta zinaweza zikabomoka na mvua ambazo zinatarajia kunyesha.
Akizungumza na wajumbe wa kamati ya maendeleo ya
kata hiyo,Mwenyekiti wa halmashauri hiyo mara baada ya kufanya ukaguzi wa
athari ya upepo huo,Makoroganya aliahidi kuwa halmashauri yake
itarekebisha madarasa hayo haraka.
“Wakati kamati ya mahafa wa wilaya chini ya mkuu
wa wilaya ikiendelea na taratibu zake za kuona namna ya kufanya sisi kwa upande
wa halmashauri,tumekubaliana kuchukua hatua za haraka za kurekebisha
madarasa yaliyoezuliwa”alisema Makoroganya.
Aliwataka wananchi walioathiriwa na upepo
huo kuwa na subira wakati serikali ikifanya tathmini halisi itakayosaidia
kujua hasara kamili ya janga hilo na kuona namna ya kuwasaidia.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD