TANGAZO
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM Rashid Chuachua (aliyesimama) kwenye moja ya mikutano yake ya kampeni mjini Masasi (Picha ya maktaba).
Na Clarence Chilumba,
Masasi.
MBUNGE wa jimbo la Mtwara vijijiji kwa tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) Hawa Ghasia ambaye pia alikuwa Waziri wa
Tamisemi serikali ya awamu nne amewaomba wakazi wa jimbo la Masasi
kumchagua mgombea ubunge wa CCM Rashidi
Chuachua kuwa mbunge wa jimbo hilo.
Ombi hilo alilitoa wilayani humo wakati alipokuwa akiwahutubia
mamia ya wakazi wa jimbo hilo kwenye mkutano wa
hadhara wa kampeni za uchaguzi mdogo
zinazoendelea jimboni hapa, ambapo mkutano huo
ulifanyika kwenye viwanja vya Terminal Two maarufu uwanja wa fisi mjini hapa.
Alisema ameamua kuja Masasi kwa lengo la
kuwaomba wananchi wa jimbo
la Masasi kwamba siku ya Desemba 20 ambapo
uchaguzi mdogo wa kuchagua mbunge wa
jimbo hilo unafanyika wamchaguwe mbunge wa chama cha mapinduzi ndiye atakaye weza kumaliza kero zao.
Alisema kwa kuwa kata jumla ya 11 kati ya 14
tayari madiwani wa CCM
wameshinda kwa kura nyingi kwenye uchaguzi mkuu
uliomalizika oktoba
25 hivyo wasikubali kufanya makosa badala yake
wamchaguwe mbunge wa chama cha mapinduzi
kuwa mbunge wao katika jimbo hilo.
Mbunge huyo aliongeza kuwa anamfahamu Chuachua
kuwa ni mtu mwenye uwezo mkubwa katika
utendaji kazi hivyo akiwa mbunge wa jimbo la Masasi ataweza kumaliza kero zote ambazo zinawakabili wananchi wa
jimbo hilo.
“Kwakuwa serikali ya CCM awamu ya tano tayari
imeshaingia Ikulu basi
nawaombeni wakazi wa jimbo la Masasi msichaguwe
mbunge wa upinzani
bali mchaguweni mgombea wa CCM ili aungane na
kasi ya Raisi Magufuli
kuleta maendeleo,”alisema Ghasia
Kwa upande wake mgombea huyo wa CCM Chuachua
alisema iwapo wananchi hao wakimchaguwa
kuwa mbunge wa jimbo la Masasi atahakikisha anafufua kiwanda cha kubangua korosho kilichopo wilayani Masasi
ili kutoa fursa za ajira kwa wakazi hao.
Aidha mgombea huyo aliongeza kwamba atasimamia
ipasavyo bei ya zao la
korosho kwa wakulima ili waweze kunufaika na
kilimo hicho ambacho ni
nyenzo kuu ya maisha kwa wakazi wa mikoa ya
kusini.
“Nawaombeni kura zenu ili niwe mbuge wa jimbo
hili nawaahidi
nitamaliza kero zenu zote naowambeni tena
nichaguweni mimi nitakuwa
mkombozi wa jimbo la Masasi,”alisema Chuachua
Chuachua alisema akiwa mbunge wa jimbo hilo
atasimamia pia mapato ya
ndani ya halmashauri yaweze kutumika kwa ajili
ya kuwaletea maendeleo
wananchi na kusisitiza kwamba suala la rushwa
kwenye halmashauri
atalishughulikia kikamilifu.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD