TANGAZO
Christopher Lilai, Nachingwea.
Baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya
Nachingwea, limemchagua Ahmadi Makoroganya kupitia CCM kuwa mwenyekiti mpya wa
halmashauri hiyo baada ya kumshinda mgombea wa CUF, Hamisi Kalembo.
Katika uchaguzi huo uliofanyika jana kwenye
ukumbi wa halmashauri,Makoroganya ambaye ni diwani wa kata ya Ugawanyaji
alipata kura 34 sawa na asilimia 72.3 na Kalembo akipata kura 13 sawa na
asilimia 27.7.
Kwa nafasi ya makamu mwenyekiti CCM iliibuka
tena kidedea baada mgombea wake Isaya Ndwewe kumshinda mgombea kupitia Chadema
,Omari Mbinga kwa kura 33 sawa na asilimia 70.2 dhidi ya kura 14
sawa na asilimia 29.8 alizopata Mbinga.
Akihutubia mara baada ya uchaguzi huo Mwenyekiti
huyo aliwataka watendaji wa halmashauri hiyo kuacha kufanya kazi kwa mazoea na
kuzingatia muda wa kazi kwani alibainisha kuwa wapo wafanyakazi ambao hawazingatii
muda wa kazi.
“Nafahamu wapo wafanyakazi wazembe ambao
wanatumia muda mwingi nje ya ofisi kwa shughuli binafsi hivyo nawataka
kubadilika na kuwa mwisho wao sasa umefika”alisema Makoroganya.
Akizindua baraza hilo, Mkuu wa wilaya ya
Nachingwea, Pololeti Mgema aliwataka madiwani hao kuacha tofauti zao za vyama
badala yake kushirikiana kuhakikisha wananchi wanapatiwa mahitaji muhimu
ikiwemo dawa, kutatua changamoto zinazowakabiliwa wananchi hasa wa vijijini.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD