TANGAZO
Mbunge wa Iramba (CCM) Mwigulu Nchemba akimnadi mgombea wa ubunge jimbo la Masasi Rashid Chuachua jana kwenye viwanja vya Kisiwani mjini Masasi.
Na Clarence Chilumba,
Masasi.
Mbunge wa Jimbo la Iramba na aliyekuwa naibu waziri wa wizara
ya fedha katika serikali ya awamu ya nne Mwigulu Nchemba amewataka wananchi wa
jimbo la Masasi kufanya siasa za amani na utulivu ili waweze kuchagua mbunge
sahihi kwa maendeleo ya jimbo la Masasi.
Nchemba aliyasema hayo jana mjini Masasi wakati anawahutubia wanachama pamona na wananchi a jimbo la Masasi kwa ujumla kwenye mkutano wa kampeni wa kumnadi mgombea wa nafasi ya ubunge kupitia CCM Rashid Chuachua.
Mkutano huo wa kampeni ulifanyika kwenye mtaa wa Kisiwani Halmashauri ya mji wa Masasi ambapo alisema Chuachua ana sifa zote za kumwezesha kuwa mwakilishi wao wa jimbo la Masasi na kwamba wasifanye makosa kupeleka bungeni mbunge asiye na sifa za kuwa mwakilishi wa wananchi.
Alisema chama cha mapinduzi kimejipanga kushinda kwenye
uchaguzi huo mdogo unaofanyika baada ya kifo cha aliyekuwa mgombea wa NLD Dk.Emanuel
Makaidi ambapo aliwataka wananchi na wanachama wa vyama vya siasa kuacha
vitendo vya vurugu wakati wa mikutano ya kampeni na hata siku ya uchaguzi.
Kwa mujibu wa Nchemba
alisema kiongozi bora ni yule anayetoka chama cha mapinduzi hivyo ni vyema
wananchi wa jimbo la Masasi wakafanya maamuzi sahihi na yaliyo bora kwa
kumchagua mgombea wa CCM Rashid Chuachua.
“Ndugu zangu wana Masasi suala la uwakilishi ni nyeti sana na
linahitaji mtu makini mwenye uwezo wa kujenga hoja kwa serikali…mchagueni
Chuachua awaletee maendeleo na mabadiliko ya kweli yatakayoendana na kasi ya
Rais Dk.John Magufuli”.alisema Nchemba.
Kwa upande wake mgombea ubunge jimbo la Masasi kupitia chama
cha mapinduzi (CCM) Rashid Chuachua aliendelea kuwaomba wananchi wa jimbo la
Masasi wamchague kwa kura nyingi ili aweze kutekeleza ahadi mbalimbali
alizoziahidi kwao wakati huu wa kampeni.
Baadhi ya Askari wa kikosi cha Green Guard wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Masasi wakipiga Push-Up nje ya ofisi ya Chama hicho wilaya ya Masasi tayari kwa mikutano ya kampeni inayoendelea mjini hapa.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD