TANGAZO
Mwenyekiti mpya wa Halmashauri ya mji wa Masasi Sospeter Nachunga akisoma dua ya Halmashauri kabla ya kikao cha baraza hilo kuanza hii leo kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.
Baraza la madiwani la halmashauri ya mji wa
Masasi mkoani Mtwara, limemchagua Sospeter Nachunga kupitia CCM kuwa mwenyekiti
mpya wa halmashauri hiyo baada ya kumshinda mgombea wa CUF, Mbwana Mkeng’endo.
Katika uchaguzi huo uliofanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri
hiyo,Nachunga ambaye ni diwani wa kata ya mpya ya Napupa alipata kura 14 na
kumbwaga mpinzani wake Mbwana Mkeng’endo aliyeambulia kura nne pekee.
Kwa nafasi ya makamu mwenyekiti CCM iliibuka
tena kidedea baada mgombea wake Ausi Mnela (kisiki cha mgomba) kumshinda
mgombea kupitia CUF, Hamza Machuma aliyepata Kura tatu pekee dhidi ya kura 15
alizopata Mnela.
Diwani wa kata ya Napupa Sospeter Nachunga akila kiapo hii leo katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya mji wa Masasi.
Akihutubia mara baada ya uchaguzi huo Mwenyekiti
huyo aliwataka madiwani kuacha kufanya kazi kwa mazoea ili kuendana na kasi ya
Rais Dk.John Pombe Magufuli kwa lengo la kuleta maendeleo kwenye kata zao.
Aidha alitoa rai kwa watendaji wa halmashauri
hiyo kufanya kazi kwa bidii ili halmashauri hiyo iwe miongoni mwa halmashauri
bora nchini huku akiwataka kuacha uzembe kazini.
“Nafahamu
wapo wafanyakazi wazembe ambao wanatumia muda mwingi nje ya ofisi kwa shughuli
binafsi hivyo nawataka kubadilika na kuwa mwisho wao sasa umefika”alisema
Nachunga.
Baraza la Halmashauri ya mji wa Masasi lina
jumla ya madiwani 18 huku madiwani 14 ni wa kuchaguliwa na wanne ni wa
kuteuliwa ambapo chama cha mapinduzi kina jumla ya madiwani 15 huku CUF ikiwa
na madiwani wawili na Chadema diwani mmoja.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Masasi Fortunatus Kagoro akizungumza wakati wa uzinduzi wa mkutano wa kwanza wa baraza la madiwani wa Halmashauri hiyo hii leo.
Diwani wa viti maalumu Christina Millanzi akila kiapo cha uaminifu kwa Halmashauri.
Diwani wa kata ya Mkuti Hamza Katani Machuma (CUF) akila kiapo hii leo.
Mbwana Mkeng'endo diwani wa kata ya Jida (CUF) akila kiapo
Wakuu wa idara na vitengo wa Halmashauri ya mji wa Masasi wakifuatilia kwa makini mkutano wa baraza la madiwani lililozinduliwa hii leo.
Diwani wa kata ya Temeke Selemani Uledi Nivako akiapa kwenye mkutano wa kwanza wa baraza ka madiwani.
Diwani wa viti maalumu Amina Chiputa akila kiapo.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD