TANGAZO
Mbunge mteule wa jimbo la Masasi kupitia CCM Rashid Chuachua akizungumza katika mahojiano maalumu na mwandishi wa Blog ya Mtazamo Mpya (Hayupo pichani) jana ndani ya ofisi ya chama hicho wilaya ya Masasi.
Na Clarence Chilumba, Masasi.
Mbunge mteule wa jimbo la Masasi
mkoani Mtwara Rashid Chuachua (CCM) amelitaka shirika
la umeme nchini tawi la Masasi kulitafutia ufumbuzi wa haraka tatizo la kukatika kwa mara kwa mara umeme ili wakazi wa jimbo hilo waweze kupata umeme wa uhakika.
Kauli hiyo imekuja baada ya suala la
umeme kugeuka kuwa kero kwa wakazi wa jimbo la Masasi na viunga vyake kutokana
na umeme huo kukatika mara kwa mara tena bila ya kuwa na taarifa yotote kwa
wateja na watumiaji wengine wa huduma hiyo muhimu.
Mji wa Masasi kwa siku za hivi karibuni umekuwa hauna umeme wa uhakika kutokana na umeme huo kukatika kila
wakati na hivyo kusababisha kupanda kwa baadhi ya bidhaa zinazotegemea nishati
hiyo ya umeme.
Akizungumza jana na Blog ya Mtazamo Mpya mara
baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa nafasi hiyo ya ubunge jimbo la Masasi
alisema kusuasua kwa huduma hiyo mjini humo kunasababisha hasara kubwa kwa
wafanyabishara ambao wengi wao hutegemea umeme kwa shughuli zao za uzalishaji
mali.
Alisema serikali imekuwa na nia
thabiti katika kutoa huduma kwa wananchi wake lakini mara kadhaa mipango ya
serikali imekuwa ikikwamishwa na baadhi ya watendaji wa serikali wakiwemo wa
shirika la umeme tawi la Masasi.
Alisema yuko mbioni kufanya
mazungumzo na mkurugenzi mkuu wa Tanesco Felschemi Mramba kuona ni kwa namna
gani tatizo la umeme linawezwa kumalizwa jimboni humo kwa kutumia gesi asilia
iliyoko mkoani Mtwara.
Alisema anazifahamu baadhi ya sababu
chache zinazosababisha umeme katika mji wa Masasi kukatika katika bila
utaratibu ikiwemo uchakavu wa miundombinu kama vile nguzo lakini ni tatizo la
muda mrefu ambalo kwa sasa lilitakiwa liwe limekwisha.
Kwa mujibu wa mbunge huyo mteule
alisema katika jimbo la Masasi viko baadhi ya vijiji havina kabisa huduma hiyo
umeme ikiwemo Matawale, Marika, Mumbaka na Temeke na kwamba tayari serikali
imeshatenga fedha shilingi Bilioni 1.17 katika kuhakikisha inasambaza umeme kwa
vijiji hivyo pamoja na vile ambavyo ni wananchi wachache tu wamepatiwa umeme.
Alisema mara atakapoapishwa
siku chache zijazo atakutana na waziri wa nishati na madini Prof, Sospeter
Muhongo ili aweze kumueleza athari za kukatika kwa umeme zinazowakumbwa wakazi
wa mji wa Masasi mji ambao kwa sasa umekuwa ukikua kwa kasi kutokana na
shughuli mbalimbali za kibiashara.
Kwa siku za hivi
karibuni wilaya ya Masasi imeingia katika tatizo kubwa la kutokuwa na uhakika
wa nishati ya umeme mazingira yanayosababisha wakazi wa mji huo kuongeza
gharama za matumizi kwa kununua majenereta ili waweze kuendesha shuguli zao za
uzalishaji mali.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD