Loading...
ADVERTISE WITH US ON THIS BLOG.CALL +255 714 789 592/ +255 682 997 767/ +255 752 944 022

VIJANA 20 KUTOKA KATIKA VIJIJI VYA MIHIMA NA SULULU WAPATIWA MAFUNZO YA KILIMO NA UFUGAJI WA KISASA.

TANGAZO
 Ofisa Kilimo wa Halmashauri ya mji wa Masasi Bw.Kalinga akitoa somo kwa vijana waliohudhuria mafunzo hayo ya kilimo yaliyofanyika katika ukumbi wa Mangonet mjini Masasi.

Na Hamisi Nasiri: Masasi.
VIJANA 20 kutoka kijiji cha Sululu na Mihima vilivyopo wilayani Masasi
mkoani Mtwara wamepatiwa mafunzo ya mbinu za kilimo na ufugaji ili
waweze kuwa na stadi endelevu za ujasiliamali hatua ambayo itawasaidia
kuweza kujikwamua kiuchumi.


Akifungua mafunzo hayo jana wilayani Masasi ambayo yametolewa na
shirika lisilo la kiserikali la MADA lililopo wilayani humo chini ya
ufadhili wa mashirika ya DSW,GIZ na Everplan, mwenyekti wa shirika
hilo Mery Chilala alisema vijana hao watafaidika na mafunzo hayo kwa
kuwa na mbinu za ujasiliamali.


Alisema mafunzo hayo yanatolewa wakati muhafaka wa kuelekea katika
msimu wa kilimo hivyo ujuzi wa masuala ya ufugaji na kilimo bora
watakaopata kupitia kwenye mafunzo hayo ya siku tatu yatawasaidia
kwenda kuanzisha shughuli za kilimo na ufugaji ili waweze kujikwamua
kiuchumi.


Mery alisema kutokana na kundi kubwa la vijana kukosa hajira shirika
hilo limeanzisha klabu mbalimbali za vijana hasa katika maeneo ya
vijijini na kuwahamasisha kushiriki katika shughuli za kiuchumi ambazo
zitawasaidia kujikwamua na umasikini na kuweza kupata kipato
kinakachowafanya waweze kumudu gharama za maisha yao.


Alisema katika kilimo vijana hao watajifunza namna ya kulima kilimo
chenye tija na kinachozingatia zana bora za kilimo sambamba na jinsi
ya kuandaa shamba na wakati gani wa kufanya maandalizi.


“Mafunzo haya yatasaidia sana kuondoa tatizo la vijana kukaa bila kazi
vijiweni na kwamba yatakuwa njia mbadala kwao katika kujikwamua
kiuchumi na kuondokana na umasikini,”alisema Mery.


Alisema pia wapatiwa mafunzo ya ufugaji rasilimali mifugo mbalimbali
ikiwemo kuku wa kisasa ambapo ufagaji huo wataweza kupata kipato na
kuelezea kuwa wapo baadhi wa watu wamefanikiwa katika maisha kwa ajili
ya shughuli za ufugaji.


Aidha Mery ametoa wito kwa vijana kuunda klabu za vijana na kujiwekea
malengo yao ikiwa na kujishughulisha na shughuli za kilimo pamoja
ufugaji ili waweze kujikwamua kimaisha.



BAADHI ya vijana waliohudhuria mafunzo hayo.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top