TANGAZO
Kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara Henry Mwaibambe akionesha baadhi ya milipuko iliyokamatwa mkoani humo.
Na Fatuma Maumba,Mtwara.
JESHI la Polisi Mkoani
Mtwara kwa kushirikiana na Marine Park pamoja na Kikosi maalum cha Taifa
kinachoshughulikia uhifadhi wa mazingira pamoja na Habari, wamefanikiwa
kukamata vifaa mbalimbali vya milipuko vinavyotumika katika uvuvi haramu wa
baruti katika bahari ya hindi katika operesheni maalum ya kuwakamata
wanaojihusisha na mtandao huo.
Akizungumza na
waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara, ACP Henry
Mwaibambe,amesema wameanzisha operesheni katika bahari ya hindi kukabiliana
na uvuvi haramu na katika operesheni hiyo wamefanikiwa kuwakamata watu watatu
vinara wa mtandao huo.
Kwa mujibu wa Kamanda
wa polisi aliwataja vinara wa mtandao huo kuwa ni pamoja na Mussa Kaisi miaka
30, mmakonde na mvuvi na, Dadi Selemani miaka 31, mmakonde, mvuvi na Hose
Chikota miaka 24 wote ni wakazi wa Naumbu wilaya ya Mtwara Vijijini
Hata hivyo Kamanda
Mwaibambe, ameomba wananchi mkoani humo kutoa ushirikiano ili kuwafichua watu
hao ambao wanaharibu mazalia ya samaki na mazingira ya habari kwa ujumla.
Kamanda Mwaibambe
amesema mtuhumiwa wa kwanza ambeye ni Mussa Kaisi alikamatwa na vifaa
mbalimbali ambavyo ni Viwashio 44, Detonator 39, Explogel-Nusu Kipande, Daftari
moja la mauzo ya vifaa hivyo, kiasi cha pesa shilingi 353,000/= na simu moja
aina ya Tecno ambayo alikuwa anatumia kwa ajili ya kuwasiliana na wateja wake
mbalimbali.
Watuhumiwa wengine
ambao walikamatwa sehemu tofauti na Mtuhumiwa wa kwanza ambao ni Dadi Selemani
na Hose Chikota ambao nao walikamatwa na malighafi za kutengenezea milipuko, walikutwa
na mbolea kilo sita kilo tatu zikiwa zimechanganywa na Explogel, chupa sita za
milipuko zilizokuwa zimesha changanywa tayari kwa kulipuliwa, waya wa vilipuzi
mita 5.5 na vitu vingine vidogo vidogo na majongoo ya bahari 55.
Watuhumiwa wote hawa
wanaendelea kuhojiwa na yatakapokamilia watafikishwa mahakamani, Jeshi la
polisi mkoa wa Mtwara wanaomba wananchi kushirikiana nao ili kuwafichua watu
hawa ambao wanaharibu mazalia ya samaki na mazingira ya bahari.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD