TANGAZO
Na Fatuma Maumba,Mtwara.
MKURUGENZI wa Bodi ya Korosho Tanzania CBT, Mfaume Juma, amesema
msimu wa ununuzi wa korosho ghafi nchini kwa mwaka 2015/2016 ulifunguliwa rasmi
kitaifa September mosi mwaka huu, ambapo mnada wa kwanza ulifanyika oktoba
mbili katika kituo cha Mtwara na kwa upande wa kituo cha mkoa wa Lindi
ulifanyika otoba 17 mwaka huu.
Aidha Mkurugenzi huyo amesema mfumo wa stakabadhi ghalani wakulima
wanakusanya korosho zao kwenye vyama vya ushirika vya msingi na baadaye maghala
makuu ambapo kupitia vyama vikuu vya ushirika chini ya usimamizi wa Bodi ya
Korosho Tanzania kwa kushirikiana na Sekretarieti ya mkoa husika korosho husika
huuzwa kwa ushindani kwenye minada inayofanyika mara moja kila wiki.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mkurugenzi huo
amesema mkoa wa Mtwara umekua wa kwanza kufanya mnada kutokana na korosho
zinazowahi kuvunwa kutoka wilaya ya Masasi.
“Ndugu wanahabari, msimu huu mnada wa kwanza ulifanyika oktoba
mbili katika kituo chetu cha Mtwara na kwa upande wa mkoa wa Lindi mnada wa
kwanza ulifanyika oktoba 17 mwaka huu katika kituo cha Lindi mjini…Mkoa wa
Mtwara umekuwa wa kwanza kufanya mnada kutokana na korosho zinazowahi kuvunwa
kutoka wilaya ya Masasi hasa maeneo yaliyo karibu na bonde la mto Ruvuma vijiji
vya Mnavira, Chikoropola na Makong’onda.
Mfaume amesema mpaka sasa wiki tano zimepita tangu minada ya korosho
ianze kufanyika msimu huu, korosho zilizokusanywa maghala makuu na kuuzwa kati
ya 0ktoba mbili hadi November 8 ni tani 57, 252.450.
“Korosho hizi zimeuzwa kwa bei za ushindani kati ya shilingi
2,407/= kwa kilo hadi shilingi 2,640 kwa kilo…Mkoa wa Lindi kwa mara ya kwanza
bei zimekuwa za ushindani mno ikilinganishwa na bei zilizopatikana mkoa wa
Mtwara.
Wakati mkoa wa Mtwara korosho zimeuzwa kwa bei kati ya shilingi
2,407/=hadi shilingi 2,620/= kw kilo mkoa wa Lindi zimeuzwa kati ya shilingi
2,563/= hadi shilingi 2,640/=kwa kilo.
Hata hivyo Mkurugenzi huyo amesema kwa ujumla soko la korosho
nchini msimu huu limekuwa la ushindani mkubwa kutokana na ongezeko kubwa la
makampuni yaliyochukua leseni “Mpaka sasa jumla ya Makampuni 110 yamechukua
leseni ikiwa ni ongezeko la asilimia 26 ikilinganishwa na makampuni
yaliyochukua leseni msimu uliopita mwaka2014/2015 tuliishia na makampuni 87 tu.
Bodi ya Korosho Tanzania kwa mara nyingine tena inapenda kutoa rai
kwa wadau wa korosho hasa Serikali za Mitaa katika maeneo yanayozalisha korosho
kushirikiana na bodi katika kukomesha ununuzi holela wa zao hilo.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD