TANGAZO
Mwenyekiti wa vyama vya ushirika wilayani ya Masasi (AMCOSS) Selemani Ndege akizungumza kwenye mahafali ya 24 ya chuo cha maendeleo ya wananchi wilaya ya Masasi siku ya ijumaa.
Na Hamis Nasiri,Masasi.
WANAFUNZI wanaosoma katika
chuo cha maendeleo ya wananchi Masasi mkoani Mtwara (FDC) hususani wasichana wameaswa kutorubuniwa kimapenzi na wananume kabla ya kuhitimu mafunzo yao kwani kwa kufanya hivyo itawasababishia washindwe kufikia malengo waliyojiwekea.
Ushauri huo ulitolewa jana wilayani humo na
mwenyekiti wa vyama vya
ushirika vya msingi (AMCOS) katika halmashauri
ya wilaya ya Masasi,
Selemani Ndege wakati alipokuwa akizungumza na
wanafunzi wa chuo hicho
kwenye mahafali ya 24 ya kuhitimu masomo yao kwa
niaba ya mwenyekiti
wa chama kikuu cha ushirika mkoani Mtwara MAMCU.
Aidha chama hicho kikuu cha MAMCU kimetoa msaada
wa shilingi Milioni tano
kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali
chuoni hapo ikiwemo ujenzi
wa mabweni.
Alisema kuwa wanafunzi wanaosoma katika chuo
hicho hasa wasichana
wasikubali kurubuniwa na wanaume kujihusisha
katika mahusiano ya
kimapenzi kwani wanaume ni waongo wanapomuhitaji
msichana kimapenzi.
Ndege alisema anatambua kuwa hadi wanafunzi hao
kuweza kuhitimu masomo
yao ya ufundi wa kushona nguo,utengenezaji wa
magari,ufundi
selemala,upishi,uashi ufundi wa umeme wa
majumbani na umeme wa magari
ni wazi kuwa wamevuka vikwazo vingi hasa kwa
wasichana.
“Sisi wanaume tumeumbwa kuwa waongo kwa nyinyi
wasichana hivyo nawaasa
wasichana msikubali kurubuniwa na wanaume someni
ili muweze kutimiza
malengo yanu,”alisema Ndege
Akisoma taarifa fupi ya chuo mkuu wa hicho, Fred
Mwakagenda alisema
chuo hicho kipo chini ya wizara ya maendeleo ya
jamii jinsia na watoto
lakini kinakabiliwa na changamoto lukuki ikiwemo
ya ukosefu wa chumba
cha kusomea (maktaba).
Alisema changamoto zingine ni ukosefu wa
karakana kwa fani mbalimbali
na kusisitiza kuwa serikali ifanye kila hali
kwenda katika chuo ili
kujionea changamoto hizo ambazo zinakwamisha
utendaji wa kazi.
Mwakagenda aliongeza kuwa jumla ya 53 wanahitimu
mafunzo yao ya miaka
miwili ambapo wanaume ni 45 na wasichana nane
wahitimu hao ni kati ya
wanachuo 81 ambao walianza chuo huku chuo hicho
kikiwa na jumla ya
wanachuo 188.
Alisema chuo cha maendeleo ya wananchi Masasi
kilijengwa mwaka 1963
kikiitwa chuo cha maendeleo ya vijijini chini ya
halmashauri ya Masasi
mwaka 1975 kilibadilishwa jina na kuitwa chuo
cha maendeleo ya
wananchi chini ya wizara ya elimu ya taifa
ambapo vilianzishwa baada
ya baba wa taifa hayati Mwalimu Julius Nyerere
kuiga vyuo vya ufundi
Sweeden Folk High School.
MKUU wa chuo cha maendeleo ya wananchi wilaya ya Masasi Fred Mwakagenda akizungumza wakati wa mahafali ya chuo hicho.
Mgeni rasmi katika mahafali hayo akioneshwa jiko linalotumia nishati ya jua na baadhi ya walimu wa chuo cha maendeleo ya wananchi-Masasi FDC.
MMOJA wa walimu wa chuo cha maendeleo ya wananchi akikata keki wakati wa maadhimisho ya mahafali hayo chuoni hapo.
BAADHI ya wanafunzi wa chuo hicho wakipokea vyeti vyao vya kuhitimu mafunzo yao chuoni hapo.
MMOJA wa wanafunzi waliohitimu akisoma risala mbele ya mgeni rasmi.
BAADHI ya wahitimu wa mafunzo hayo chuoni hapo.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD