TANGAZO
Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Masasi Fortunatus Mathew Kagoro.
TAARIFA
KWA WAKAZI WA JIMBO LA MASASI
Msimamizi wa uchaguzi jimbo
la Masasi anawatangazia wananchi wote kwamba kampeni za uchaguzi wa nafasi ya
ubunge jimbo la Masasi zitaanza rasmi Novemba 15,2015 hadi Desemba 19,2015 na
uchaguzi utafanyika Desemba 20,2015.
Uchaguzi huu unafanyika
baada ya aliyekuwa miongoni mwa wagombea wa nafasi hiyo ya ubunge kwa jimbo la
Masasi kupitia chama cha NLD Dk.Emanuel John Makaidi kufariki dunia Oktoba 15,
2015 huko katika Hospitali ya Misheni ya Mtakatifu Walburger Nyangao mkoani
Lindi kutokana na tatizo la shinikikizo la damu.
Kwa upande wa chama cha NLD
kitafanya uteuzi wake wa kumpata mrithi wa Dk.Makaidi atakayepeperusha bendera
ya chama hicho na hatimaye jina hilo kuwasilishwa kwa msimamizi wa uchaguzi Novemba
14, 2015 kabla ya saa 10:00 jioni.
Tayari vyama vinne
vimewasilisha majina ya wagombea wao watakaowania nafasi hiyo ya ubunge jimbo
la Masasi ambao ni:
1. Rashid Chuachua-CCM
2. Ismail Makombe
(Kundambanda)-CUF
3. Mustapha Swalehe-CHADEMA
4. Dk.Peter Timothy
Omari-ACT-WAZALENDO.
Msimamizi wa uchaguzi jimbo
la Masasi anaendelea kutoa wito kwa wananchi wote wa jimbo hilo kushiriki
kikamilifu kwenye zoezi zima la kampeni mpaka siku ya uchaguzi kwa amani na
utulivu kama ilivyokuwa hapo mwanzo wakati wa uchaguzi wa Rais na madiwani
uliofanyika oktoba 25,2015.
Imetolewa na Idara ya Habari,Mawasiliano na
Mahusiano,
S.L.P.447,
Simu: 023 - 2510685,
E-Mail:masasitc@mtwara.go.tz
Website:www.masasitc.go.tz
Halmashauri ya mji wa Masasi-Mtwara.
Tarehe 10, Novemba 2015.
Simu: 023 - 2510685,
E-Mail:masasitc@mtwara.go.tz
Website:www.masasitc.go.tz
Halmashauri ya mji wa Masasi-Mtwara.
Tarehe 10, Novemba 2015.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD