TANGAZO
Moja ya Mradi wa barabara unaotekelezwa na Halmashauri ya mji wa Masasi mkoani Mtwara.
Halmashauri ya mji wa Masasi mkoani Mtwara iko mbioni kukamilisha ujenzi wa barabara ya kiwango cha Lami yenye urefu wa kilometa 1.15 inayotoka eneo la TK kuelekea REST CAMP barabara itakayogharimu fedha za kitanzania shilingi Milioni 350.
Ujenzi wa barabara hiyo ya kiwango cha Lami ulianza June 2015 na unatarajia kukamilika Desemba 2015.
Kampuni inayojenga barabara hiyo ni kampuni ya Wazawa kutoka Masasi ya Wanyumbani Construction Company Limited (WCCL) ambapo msimamizi wa mradi huo ni Mhandisi wa Halmashauri ya Mji wa Masasi Injinia Silaji Mbuta.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD