TANGAZO
Ujenzi wa Barabara ya kiwango cha Lami inayojengwa wilayani Ruangwa yenye urefu wa kilometa 2.5 ukiwa unaendelea.
Huu ni moja ya mradi ambao utasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa changamoto kadhaa ambazo zilikuwa zinaikabili wilaya hiyo kutokana na tatizo la barabara ambalo ni kiungo muhimu kwa maendeleo ya wilaya hiyo.
Baadhi ya wananchi wilayani humo wameelezea namna ujenzi wa barabara hiyo utakavyosaidia kufungua fursa mbalimbali kwa wafanyabiashara wa mazao ambao wengi wao hutumia barabara hiyo kusafirisha bidhaa mbalimbali.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD