TANGAZO
Katibu wa chama cha Mapinduzi mkoa wa Mtwara Shaibu Akwilombe akimnadi mgombea wa ubunge jimbo la Masasi Rashid Chuachua.
Na Clarence Chilumba,
Masasi.
MGOMBEA wa nafasi ya ubunge
kupitia chama cha mapinduzi (CCM) jimbo la Masasi Rashid Chuachua amewaahidi
wananchi wa mji wa Masasi na viunga vyake kuwa endapo watampa ridhaa ya kuwa
mbunge wao atajenga stendi mpya ya mabasi katika mji huo.
Uchaguzi huo mdogo wa ubunge katika jimbo la Masasi unatarajia kufanyika Disemba 20 mwaka huu kutokana na kushindwa kufanyika oktoba 25 baada ya mgombea ubunge wa chama cha NLD Dk.Emanuel John Makaidi kufariki dunia oktoba 15 katika hospitali ya misheni ya Nyangao mkoani Lindi kutokana na tatizo la shinikizo la damu.
.
Aidha amewaomba wamchague ili
aweze kuboresha sekta ya kilimo kwa kurasimisha ardhi ya wakulima waweze kupata
hati za kimila zitakazowawezesha kupata mikopo kwenye taasisi za kifedha.
Akihutubia leo maelfu ya wananchi wa jimbo la Masasi wakati
wa mkutano wa kampeni za chama hicho zilizofanyika katika viwanja vya Terminal two
(Uwanja wa Fisi) mjini humo alisema
anafahamu kero walizonazo wananchi wa jimbo la Masasi ikiwemo stendi kuu ya
mabasi ambayo haina hadhi ya mji wa Masasi.
Amesema uwepo wa stendi kuu
ya mabasi ya kisasa kutaongeza mapato kwa halmashauri kutokana na kodi kutoka
kwa wafanyabiashara na wamiliki wa mabasi hayo watakaolaza mabasi yao ndani ya
stendi hiyo.
Kwa mujibu wa mgombea huyo
alisema endapo wananchi wa jimbo la Masasi watampa ridhaa hiyo ya kuwa mbunge
wao atashirikiana na wadau mbalimbali wa ndani na nje katika kufanikisha ujenzi
wa stendi mpya na ya kisasa.
“Ndugu zangu kwa sasa mji
wetu wa Masasi hauna stendi ya kisasa inayoendana na hadhi ya mji wetu…hivyo
nawaomba ifikapo desemba 20 mnipe kura nyingi za ndio ili niweze kutekeleza kwa
vitendo ahadi zangu ikiwemo hii ya stendi”.alisema Chuachua.
Akizungumzia kuhusu taarifa zinazosambazwa na wapinzani wake kuwa
yeye si mzaliwa wa wilaya ya Masasi alisema,wananchi wasipotoshwe na uvumi huo
na kwamba yeye ni mzaliwa wa wilaya ya Masasi huku akiwataka wananchi kumpinga
kiongozi anayetaka kuchaguliwa kwa kigezo cha ukabila,udini na ukanda.
Pia amehaidi kushughulikia
matatizo ya watumishi wa sekta ya afya ambao wamekuwa wakishindwa kupewa
stahili zao kwa wakati licha ya umuhimu wa kazi yao kwa jamii huku akiweka wazi
dhamira yake ya kuwa mbunge mwenye nia thabiti ya kupambana na umaskini.
Mkutano huo wa
kampeni ni mwendelezo wa harakati za kampeni zilizoanza kutimua vumbi Novemba
15 mwaka huu na zinatarajiwa kukamilika Desemba 19 ambapo katika mkutano huo wa
leo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho akiwemo mbunge wa jimbo
la Mtwara Vijijini Hawa Ghasia.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD