TANGAZO
Katibu mkuu wa wizara ya afya na ustawi wa jamii Dk. Donan Mmbando.
SERIKALI imesema ipo katika hatua za
mwisho kuanzisha maduka ya dawa katika hospitali zake zisizokuwa nayo na kuweka
maduka mapya ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD), hatua itakayohakikisha dawa
zinapatikana katika hospitali hizo.
Aidha, imesema ili
kufanikisha hilo, inafanya mazungumzo na wamiliki binafsi wa maduka ya dawa
yaliyo nje ya hospitali zote za serikali ili yahamishwe kuondoa mgongano wa
kimaslahi baada ya kubaini maduka mengi ni ya watumishi wa afya.
Katibu Mkuu wa Wizara
ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Donan Mmbando, aliyasema hayo jana,
alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kufanya ziara katika Hospitali ya
Saratani ya Ocean Road na kufafanua zaidi kwa simu alipozungumza na gazeti hili
baada ya ziara hiyo.
Dk Mmbando alisema
changamoto ya dawa ipo katika maeneo mengi ya nchi, hivyo serikali imeandaa
utaratibu wa kuweka maduka ya dawa ya serikali ndani ya hospitali zake ambayo
yatasaidia upatikanaji wa dawa kwa wepesi na kwa bei rahisi. “Maduka ya dawa
hayapo katika hospitali zote.
Tuliruhusu kuwepo kwa
maduka binafsi ili kuongeza ushindani wa dawa, lakini baadhi ya watumishi wasio
waaminifu wanawaandikia wagonjwa dawa wanazojua katika duka la hospitali
hakuna, na kumwagiza aende duka la nje ambalo ni lake ama la mwenzake.
“Mpango tunaouzungumza
hapa ni kuweka maduka katika hospitali za serikali zisizo nayo na pia kuanzisha
maduka ya MSD ndani ya hospitali moja kwa moja ili kuhakikisha dawa stahiki
zote zinapatikana kwa wakati,” alifafanua Dk Mmbando.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD