TANGAZO
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Ban Ki-Moon.
KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban
Kimoon ameeleza imani yake kwa Rais John Magufuli akisema chini ya uongozi
wake, Serikali ya Tanzania itashughulika na juhudi za kuondoa umaskini,
kuimarisha utawala na kupigania amani na utulivu katika Afrika Mashariki na nje
ya ukanda.
Aidha, Mtendaji huyo wa
Umoja wa Mataifa, amesema ana imani kuwa masuala ya uchaguzi yaliyobakia
yatashughulikiwa kupitia taratibu za kisheria zilizopo kwa njia ya amani na
uwazi.
“Napenda kukuhakishia
kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea kukuunga mkono pamoja na Serikali yako katika
juhudi hizi,” alisema Ban kwenye barua yake ya pongezi aliyomtumia Dk Magufuli
kutokana na kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Tano wa Tanzania mwishoni mwa mwezi
uliopita.
Akizungumzia Uchaguzi
Mkuu wa mwaka huu, Ban alisema ni uthibitisho wa wazi na dhamira ya muda mrefu
inayoonesha demokrasia, amani na utulivu wa Watanzania. “Nina imani kuwa
masuala ya uchaguzi yaliyobakia yatashughulikiwa kupitia taratibu za kisheria
zilizopo kwa njia ya amani na uwazi,” alisema Katibu Mkuu wa UN.
Ingawa hakutaja moja
kwa moja masuala ya uchaguzi yaliyobakia, Mtendaji huyo wa UN alimaanisha
uchaguzi wa Zanzibar ambao Tume ya Uchaguzi (ZEC) ilifuta matokeo yake baada ya
kubaini kasoro kadhaa. Katibu Mkuu huyo wa UN ameipongeza Tanzania kwa kuwa
mwenza imara na wa kutumainiwa wa Umoja wa Mataifa kwa miongo yote.
“Nathamini ushirikiano
uliopo baina ya Umoja wa Mataifa na nchi yako na katika kuendeleza malengo ya
UN, nakutakia mafanikio katika kutekeleza shughuli zako,” alisema.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD