TANGAZO
Kamishna Mkuu wa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Rished
Bade.
ISO 9001:2008 CERTIFIED
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA YA MAKUSANYO YA
KODI
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
imekusanya jumla ya shilingi trililion 3.77 kuanzia mwezi Julai hadi Oktoba
2015 ambayo ni sawa na asilimia 97.6. ya lengo la makusanyo ya sh trilioni 3.87
ikiwa ni jitihada za TRA kutekeleza mkakati wa serikali ambao unaitaka
kukusanya Ths . Trililioni 12.3 kwa mwaka wa fedha 2015/2016.
Kwa mujibu wa Kamishna
Mkuu wa TRA Rished Bade, mwezi Julai TRA ilikusanya kiasi cha shilingi bilioni
849,582.9 ambacho ni asilimia 99.4 ya lengo la kukusanya shilingi bilioni
854,922.9.
Mwezi Agosti TRA
ilikusanya kiasi cha shilingi bilioni 890,536.7 ambacho ni asilimia 101.5 ya
lengo la kukusanya shilingi biilioni 876,974.2 .ambapo mwezi Septemba jumla ya
shilingi trilioni 1,067,888.3 zilikusanywa ikiwa ni asilima 91.7 ya lengo
trilioni 1,163,999.4 kwa mwezi mwezi Oktoba TRA iilkusanya shilingi bilioni
970,089.6 ikiwa ni asilima 99.3 ya lengo la kukusanya shilingi bilioni
976,441.5.
Taarifa ya mwenendo wa
makusanyo ilipitishwa na Bodi ya Wakurugenzi ya TRA katika kikao cha bodi
kilichofanyika jana tarehe 10 Novemba 2015 katika ofisi za makao makuu ya TRA”
amesema Bw. Bade.
Mafanikio katika
makusanyo haya yametokana na mikakati madhubuti iliyowekwa na mamlaka baada ya
kusaini mkataba na Waziri wa Fedha ambapo Kamishna Mkuu alisaini mkataba na
kila Mkuu wa Idara na wakuu wa Idara kusaini mikataba na wafanyakazi walioko
chini yao ili kila mfanyakazi kuwajibika ipasavyo.
Wito wa TRA ni kwa
mfanyabiashara na wadau wote wa kodi kutimiza wajibu wao wa kulipa kodi kwa
hiari ili kuchangia pato la taifa.
Sambamba na hilo TRA
imepokea kwa furaha sana wito wa Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli wa
kuhimiza ukusanyaji wa mapato bila woga na bila kumwonea mtu.
“Pamoja Tunajenga Taifa Letu”
“Pamoja Tunajenga Taifa Letu”
Rished Bade
KAMISHNA MKUU.
KAMISHNA MKUU.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD