TANGAZO
Baadhi ya wanakikundi cha Ushirika Women Group wakiwa ukumbi wa chakula uliopo kwenye kituo cha watoto mahitaji maalumu kilichopo katika shule ya msingi Masasi Halmashauri ya mji wa Masasi hii leo waliopoenda kutoa msaada.
Na Clarence
Chilumba,Masasi.
Akinamama wanaounda kikundi
cha Ushirika Women cha wilayani Masasi mkoani Mtwara wametoa msaada wa chakula
na vifaa mbalimbali kwa watoto wenye mahitaji maalumu katika shule ya msingi ya
Masasi Halmashauri ya mji wa Masasi.
Msaada huo umetolewa leo
shuleni hapo na baadhi ya wanachama wa kikundi hiko ambapo msaada huo wenye
thamani ya zaidi ya shilingi milioni moja ni pamoja na
unga,sukari,sabuni,mafuta ya ngozi kwa watoto wanaoishi na ualbinism,vifaa vya
kujifunzia na kufundishia,vinywaji pamoja na mafuta ya kupikia.
Akizungumza leo wakati wa
makabidhiano ya msaada huo mwenyekiti wa Ushirika Women Group Esther Kiwona
alisema lengo la msaada huo ni kuonesha mfano kwa makundi mengine wilayani
Masasi na Tanzania kwa ujumla kuona umuhimu wa makundi haya ya watoto wenye
mahitaji maalumu katika jamii kwani wao pia ni watoto kama walivyo watoto
wengine.
Alisema kikundi chao cha
ushirika kinaundwa na wanachama 13 ambao kwa nyakati tofauti wamekuwa
wakishangishana fedha wenyewe na kwamba baadhi ya fedha inayopatikana hutumika
kutoa misaada mbalimbali kwa jamii wilayani Masasi katika sekta za afya,elimu
na maji.
Alisema kwa nyakati tofauti
kikundi hicho kimetoa misaada katika hosiptali ya Mkomaindo mjini Masasi na kwa
watoto wenye mahitaji maalumu wilayani Masasi huku akieleza changamoto kubwa
inayowakabili kwa sasa ni kukosa vituo maalumu vinayolea watoto wenye mahitaji
maalumu na badala yake wamelazimika kurudi tena kwenye shule hiyo ambayo tayari
walishatoa msaada kipindi cha nyuma.
Kwa mujibu wa mwenyekiti
huyo alitoa wito kwa jamii kutembelea kituo hiko ili wajionee changamoto
mbalimbali wanazokumbana nazo watoto hao pamoja na walimu wao ili waweze kutoa
misaada mbalimbali itakayosaidia kuinua ari ya kujisomea na hatimaye watoto hao
waweze kufanya vizuri kwenye mitihani yao.
Kwa upande wake mkuu wa
kituo hiko cha kulelea watoto wenye mahitaji maalumu Mwanaidi Mtaka alisema
kituo chake kina wanafunzi 73 ambao wako kwenye makundi mbalimbali ya walemavu
ikiwemo wasioona,viziwi wasioona,walemavu wa viungo,wenye huoni hafifu pamoja
na wale wanaoishi na ualbinism.
Alisema kitendo
kilichofanywa na kikundi hiko kuleta msaada shuleni hapo ni cha kiungwana na
kinapaswa kuigwa na watanzania wote huku akiwaomba jamii kujitokeza kutoa
misaada mbalimbali kwa watoto hao wenye mahitaji maalumu ili nao wajisikie kuwa
nao ni sehemu ya jamii inayowazunguka.
Akizungumzia kuhusu
changamoto zinazoikabili shule hiyo alisema ni pamoja na uzio imara wa
kuzunguka mabweni shuleni hapo,chakula,vifaa vya kufundishia na kujifunzia pamoja na miundo mbinu rafiki kwa wanafunzi
hao ikiwemo madarasa,vyoo,vyumba maalumu vya kusomea pamoja na miundo mbinu ya
maji.
“Ndugu zangu binafsi na kwa
niaba ya walimu pamoja na wanafunzi wa shule yetu…napenda kuwapongeza na
kuwashukuru kwa moyo wa kizalendo mliotuonesha mpaka mkaamua kuleta msaada kwa
watoto hawa,ukweli ni kwamba msaada huu umekuja wakati muafaka na nawaomba
msichoke kuja tena kwetu kutupatia msaada”.alisema Mtaka.
Nae mkuu wa kitengo cha
watoto wenye mahitaji maalumu mwalimu Abunuasi Nampoto alisema ni mara chache
sana kwa watanzania kuweza kutoa msaada kwa makundi maalumu kama walivyofanya
kikundi cha Ushirika na kwamba jamii inapaswa kutambua umuhimu wa kundi hili la
mahitaji maalumu.
Wana Kikundi cha Ushirika Women Group cha wilayani Masasi wakishusha vifaa mbalimbali baada baada ya kuwasili shuleni hapo.
Mwenyekiti wa Ushirika Women Group Esther Kiwona akizungumza na mmoja wa watoto wanaoishi na ualbinism katika kituo cha kulelea watoto hao kilichopo eneo la Mtandi mjini Masasi.
Watoto wenye wenye mahitaji maalumu wakiwa kwenye picha ya pamoja na wana kikundi wa Ushirika women Group waliotembelea shuleni hapo kwa ajili ya kutoa msaada.
Katibu wa Ushirika women Group Caroline Karonga akimkabidhi mfuko wa unga mmoja wa wanafunzi wenye mahitaji maalumu shuleni hapo.
Mwenyekiti wa Ushirika Women Group Esther Kiwona akimkabidhi mtoto mwenye ualbinism mafuta ya ngozi yanayotumika kupaka kwenye miili yao.
Baadhi ya msaada wa vifaa mbalimbali vilivyotolewa kwa wanafunzi wa shule watoto wenye mahitaji maalumu na kikundi cha ushirika Women.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD