TANGAZO
Jaji Damian Lubuva,Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
TUME ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) imeandaa vituo vya kupigia kura 64,736. Kati ya hivyo, Tanzania
Bara ina vituo 63,156 na Zanzibar 1,580 na kila kituo kimepangwa kuwa na uwezo
wa kuhudumia wapiga kura 450 na wasiozidi 500.
Akizungumza
katika mkutano wa NEC na viongozi wa vyama vya siasa jana mjini Babati mkoani
Manyara, Ofisa Mwandamizi wa NEC, George Kashura alisema kituo kinapokuwa na
wapiga kura zaidi ya 500, kitalazimika kugawanywa na kuwa A na B ambapo namba
ya wapiga kura itakuwa nusu kwa nusu.
Alisema
ni muhimu vyama vya siasa nchini vikahamasisha wapiga kura kwenda katika vituo
walivyojiandikisha kupiga kura, siku nane kabla ya siku yenyewe ili kufahamu
vituo vyao halisi. Alisema ili kuleta mafanikio katika uendeshaji wa uchaguzi
ujao vyama vya siasa vina nafasi kubwa katika kuelimisha na kuhamasisha jamii.
“Hamasisheni
wananchi kujitokeza kushiriki uchaguzi Mkuu Oktoba 25. Tume imejipanga
kuhakikisha kila mpiga kura mwenye sifa za kupiga kura anapiga kura yake pasipo
kubughudhiwa, wanaoishi na ulemavu, wasioona tumeandaa vifaa maalumu ili waweze
kupiga kura,” alisema.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD